 |
Cristiano Ronaldo |
Klabu mbalimbali barani Ulaya zimeonesha nia ya kumsajiri winga wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo mara tu baada ya Ronaldo kutangaza kuwa hafuraii maisha katika klabu hiyo na kuna kundi la wachezaji ambao hawapendi uwepo wake hapo Madrid.Cristiano Ronaldo ambaye ana umri wa miaka 27 bado hajatoa uamuzi wa ama kuhama klabu hiyo au kubaki lakini mengi yatajulikana ya kuwa ni kwa nini Ronaldo hafurahishwi na maisha ya sasa katika klabu hiyo ya Madrid.Vilabu vinavyonyatia sahihi ya mchezaji huyo wa Ureno ni pamoja na PSG,Chelsea na Manchester City.Lakini taarifa zilizotoka hivi karibuni zinasema kuwa mkurugenzi wa klabu ya PSG Leonardo amekanusha kuwepo na taarifa za mchezaji huyo wa Ureno kuhusishwa na kwenda Ufaransa kunako klabu hiyo ya PSG.
0 comments:
Post a Comment