
Akisubiri kusikiliza kesi inayomkabili ya ubaguzi wa rangi dhidi ya beki wa QPR Anton Ferdinand,nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama 'The Three Lions' ametangaza kutoichezea tena timu ya taifa ya Uingereza kwa lugha nyingine ametangaza kustaafu.Uamuzi huo wa Terry umekuja wakati ambao yeye mwenyewe anaamini kuwa chama cha mpira wa miguu FA kina njama ya kuhakikisha kinampa adhabu kutokanan na kitendo hicho(cha ubaguzi) ambacho Terry anaamini hakukifanya.
Terry mwenye umri wa miaka 31anasema "nadhani FA watakuwa na jambo ambalo silielewi.Tayari mahakama ilishaniachia huru ila nashangaa FA wana kitu gani na mimi."Na akizungumzia uamuzi wake wa kustaafu timu ya taifa anasema,"nilikuwa na ndoto za kuichezea timu ya taifa tangu mdogo.Nimekuwa nikijitoa kwa ajili ya timu na nilichezea timu ya taifa kwa mapenzi yote.Namtakia mafanikio tele kocha Roy pamoja na wachezaji wenzangu wa timu ya taifa.

Terry anasema kuwa FA imeshindwa kutafsiri sheria namba 6.8 ya makosa ya jinai inayosema"matokeo na ushahidi wa kweli wa kesi ya jinai inabidi kuchukuliwa kama ndiyo uamuzi sahihi wa kesi husika" anasema Terry.
Wasifu wa John Terry kwa ufupi.
- Alizaliwa Disemba 7 katika jiji la London(Uingereza) mwaka 1980.
- Mwaka 1998 aliichezea klabu yake ya Chelsea mechi ya kwanza dhidi ya Aston Villa.
- Mwezi Juni mwaka 2003 aliichezea timu ya taifa ya Uingereza mechi ya kwanza dhidi ya Serbia na Montenegro akitokea benchi.
- Mwaka 2006 mnamo tarehe 10 mwezi wa nane alichaguliwa kuwa nahodha wa timu ya taifa kuchukua mahala pa David Beckam na aliyekuwa kocha Steve McClaren
- Mwaka 2008 alichaguliwa kuwa nahodha wa kudumu na aliyekuwa kocha Fabio Capello.
- Mwaka 2009 tarehe 20 Disemba klabu ya Chelsea inamtetea Terry kwa kuhusika na kuchukua hela kinyemela katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo huku kesi hiyo ikihusishwa na utovu wa nidhamu.
- Mwaka 2010 John Terry avuliwa unahodha na kocha Fabio Capello.Pia akumbwa na kashfa ya kutembea na mpenzi wa rafiki yake na mchezaji mwenzake Wayne Bridge.Msichana huyo alitambulika kwa jina la Vanessa Perroncel .
- Mwaka 2011 arudishiwa unahodha na kocha Fabio Capello.Tarehe 23 Oktoba atoa taarifa ya kukanusha kumbagua beki wa QPR Anton Ferdinand.Tarehe 21 Disemba mahakama yamkuta Terry na hatia hivyo kumfungulia kesi ya jinai.
- Mwaka 2012 Februari 3 bodi ya chama cha soka Uingereza FA inamrudishia unahodha Terry bila kumhusisha aliyekuwa kocha wa timu ya taifa Fabio Capello.
- Februari 8 Capello anajiuzulu timu ya taifa baada ya kugundua kuwa Terry alirudishiwa unahodha kinyemela pasipo kushirikishwa.
- Mahakama ya westminister inamwachia huru kutokana na kesi ya ubaguzi dhidi ya Anton Ferdinand wa QPR.
- July 27 FA yamhusisha Terry katika kutoa maneno ya kibaguzi kwa Anton Ferdinand.
- Tarehe 23 mwezi septemba anajiuzulu kuichezea timu ya taifa.
0 comments:
Post a Comment