
Manchester United wanaweza wakawa wamemnunua Robin Van
Persie kwa £24,Chelsea
wamemnunua Eden Hazard kwa £32 ,Oscar kwa £ 25 lakini Santiago Rodriguez Carzola hakika Arsenal wameizulumu Malaga.Ameigharimu
arsenal kiasi cha £15 na hayo sio maneno yangu ni maneno ya kiungo wa Swansea
Miguel Perez Cuesta a.k.a Michu kiungo ambaye amecheza na Carzola kweye Shule
ya soka ya Oviendo. Achilia mbali Mbali uwezo wake wa kuusoma mchezo,kukimbia
na mpira umbali Fulani,kupiga mashuti yanayolenga lango,kuwa na muono na pasi
sahihi pamoja na stamina ya kutosha lakini kubwa ni kuweza kufanya haya yote
kwa kutumia miguu yake yote kwa 100%.
Achilia mbali ubahiri wa mzee Wenger lakini kwangu Carzola
anabaki kuwa mchezaji bora katika ligi kuu ya premier aliyesajiliwa msimu
huu.Soka la Ulaya siku hizi limeharibiwa na pesa lakini kama umetazama mchezo
wa jana baina ya Arsenal na Manchester City unaweza ukapanga mwenyewe Carzola anunuliwe na alipwe kiasi gani lakini sio £15
pesa iliyomleta Alex-Oxlade Chamberlain Arsenal.Ubora wake huwezi kuutofautisha
na wa Yaya Toure na David Silva
wanaolipwa £200,0000 kwa juma na kuna baadhi ya vitu ambavyo
vinamtengeneza Carzola hawana.

Huyu jamaa ni hatari sana na bahati nzuri amekutana na mtu
mwingine hatari vile vile Profesa anayeweza kujua wapi mchezaji sio tu atacheza
bali atacheza na kuweza kupata ujazo wa kipaji chake na huyu si mwingine ni
mzee Wenger. Carzola mwenyewe anasema nilijua nakuja kucheza pembeni kama nilivyozoea lakini nimewekwa sehemu ambayo nahisi
nilipaswa kucheza wakati wote huko nyuma.Carzola muda wote wa kucheza soka
amecheza sana pembeni lakini kwa sasa anaecheza akiwa mchezaji huru uwanjani
eneo ambalo zamani alikuwa akicheza Fabregas.

Santiago Carzola sio tu kwamba amewafanya Arsenal wamsahau
Cesc Fabregas aliyetimkia Barcelona lakini pia ameongeza ubora kwenye kiungo ya
Arsenal na kuwafanya wawe katika nafasi nzuri ya kumaliza ukame wa vikome
Emirates. Kurejea kwa Jack Wilshere,Abou Diaby,Thomas Rosicky, Emanuel Frimpong
na uwepo wa Mikel Arteta,Aaron Ramsey,Frasis Cocuelin na Alex Oxlade
Chamberlani kumemfanya Wenger kufika hatua ya kusema kwa ubora na idadi ya
viungo nilionao ni mchanganyiko ambao sijawahi kuuona wala kuwa nao muda wate niloishi hapa.
0 comments:
Post a Comment