Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, September 6, 2012

ROONEY:GOLI LANGU LILIZIMA KELELE ZA JIRANI




 

Wayne Rooney akielezea goli lake katika kitabu chake alichokizindua hivi karibuni kinachoitwa My decade in the premier league ambacho mwendelezo wake unachapishwa pia  na gazeti  la the mirror.Rooney maarufu kama “Wazza” alifunga goli hilo dhidi ya wapinzani wao wakubwa katika jiji la Manchester na hao sio wengine ni Manchester City.Hakika lilikuwa ni goli bora kabisa sio kwa Rooney pekee bali pia kwa Manchester  United lakini pia hata kwa ligi kuu yenyewe pale nchini Uingereza. Ilikuwa ni mwezi wa pili dakika ya 77 mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza na timu ya Manchester United alipofunga goli hilo maarufu kama tik-tak na kuipa timu yake ushindi wa 2-1.

Rooney anasema goli lile ilikuwa ni tamu na ni maalumu kwa majirani zetu wanopiga makelele.Utamu wa goli lenyewe sio tu kwamba unachagizwa na mechi ya baina ya watani wa jadi bali ni ukweli kwamba lilikuja wakati ambao Rooney ametoka kushusha presha za mashabiki miezi miwili iliyopita  baada ya kusaini mkataba mpya baada  takribani juma zima kuhusishwa na kuihama  United.Anaendelea anasema hisia za kuifungia Manchester united goli kama lile mara zote huwa ni kubwa sana lakini ni kubwa zaidi kwasababu nimewafunga Manchester City.Ansema jinsi nilivyojisijisikia kama ningepata nafasi ningejitengenezea kinywaji chenye nguvu sana mfano wa konyagi hivi au banana kwa hapa kwetu sijui kwao ingekuwa nini.

Ansema mara nikahisi mapigo yangu ya moyo yananienda mbio mara nikahisi yamerudi katika hali yake naona kila kitu kipo sawa ila nasikia sauti kubwa inayoumiza masikio yangu jasho linashuka kwenye shingo yangu na huku jezi yangu ukiwa imejaa matope,mara naskia makelele juu yangu mara watu wanavuta jezi yangu na mapigo ya moyo nayo yakienda yakiongezeka kifuani kwangu.Nasikia mashabiki wakiimba jina labu Rooney Rooney Roooney Roooonee- Rooney na hakika hakuna hisia bora duniani kama hizi.

Anendelea anasema niliposimama huku kichwa kimetazama juu na mikono yangu nimeitawanya nasikia makelele na maneno ya chuki kutoka kwa mashabiki wa Manchester City yalikuwa ni kama umeme ambao hauzunguki yalikuwa na maneno makali yaliyochanganyika na matusi kebehi na vitisho mbali mbali lakini sikujali sana kwasababu najua kiasi gani wananichukia na hata mimi najisikia vivyo hivyo pindi ninapofungwa. Lakini mimi ni Wayne Rooney nimecheza ligi kuu kwa miaka kumi sasa tangu 2002 kwa hiyo nina uzoefu lakini kikubwa nimefunga  goli bora na muihimu pengine kuliko yote msimu mzima kwa upande mwekundu wa mji na kuwatahadharisha na wapinzani wengine kwamba tunaenda kuchukua kombe lingine.

 




0 comments:

Post a Comment