ASAMOAH ANA NAFASI KATIKA KIKOSI CHA JUVENTUS?
Klabu ya Juventus imefanya usajiri
wa wachezaji kadhaa msimu huu wa Serie A kama Mauricio Isla,Nicola
Leali,Richmond Boakye na bila kmsahau kiungo mchezeshaji Kwado
Asamoah.Wachambuzi wengi wa mambo na wapenzi wa Juventus wanajiuliza kuwa Je,Kwado
Asamoah ataweza kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Juventus?na Je,nafasi
yake katika kikosi cha Juventus ipoje?
Kwa walioitazama mechi ya Supercoppa
Italiana kati ya Juve na Napoli watakubaliana na mimi kuwa Kwado Asamoah ameleta
changamoto mpya katika kiungo cha Juventus ambacho kwa muda mrefu sasa kimekuwa
na viungo bora kabisa watatu Ulaya ambao ni Arturo Vidal,Andrea Pirlo na
Claudio Marchisio.Ujio wa Kwado pia utalifanya Juve iwe na uchaguzi wa mifumo
mbalimbali tofauti na wa sasa unotumika mpaka na kocha anayeshikilia nafasi ya Antonio
Conte ambaye amefungiwa na chama cha mpira wa miguu nchini Italia(FIGC)
namzungumzia Massimo Carrera.
Nilikuwa nikijiuliza pia kuwa
itakuwaje kama kiungo maestro Andrea Pirlo ambaye anaonekana kama uti wa mgongo
wa klabu hiyo ya Turin anakosekana katika kiungo cha Juventus?Je,Juve watakuwa na nguvu ama uwezo kama walionao
wakiwa na kiungo huyo?Nasema hivyo kwa sababu Pirlo alicheza mechi 37 katika
msimu uliopita wa Serie A katika umri wake wa miaka 34.Na alionekana kuwa na
msaada mkubwa sana katika kiungo cha Juve pamoja na kuwepo kwa viungo wengine
kama Simone Padoine,Emanuel Giacherrine,Arturo Vidal na Claudio Marchisio.
Kwa kipindi kirefu sana klabu ya
Juventus haijapata mchezaji wa kariba ya Asamoah hasa katika idara ya kiungo
ambaye atakuwa na uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani na wakati huo
huo akiwa na uwezo wa kupiga pasi katika ile robo tatu ya lango la timu
pinzani.Si Arturo Vidal,Marchisio wala Pirlo wenye uwezo wa kucheza nafasi
zaidi ya moja kama aliokuwa nao Asamoah na hivyo Asamoah kujidhiirisha kuwa ni
mmoja kati ya wachezaji bora ambao Juve wamewasajiri msimu huu.
Uwezo wa Asamoah unafananishwa na
uwezo wa wachezaji waliopita katika klabu hiyo kama Edgar Davis na Didier Deschamps
ambao walikuwa na uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani.Kwa mfano
Edgar alikuwa na uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto vizuri,kama kiungo
mkabaji,kama kiungo wa kati na kama winga pale ilipolazimu.
Add caption |
Asamoah
ni aina ya viungo wanaoweza kusogea toka eneo alilopangiwa katika majukumu
uwanjani mpaka katika maeneo ya hatari ya timu pinzani na hivyo kumfanya awe
katika nafasi nzuri sana katika kupata nafasi kikosi cha kwanza cha klabu hiyo
maarfu kama La Vecchia Signora(Kibibi kizee cha Turin).Asamoah anakumbukuwa mno
na mashabiki wa klabu ya Udinese maarufu kama Pundamilia wadogo(Zebrette) kwa
namna alivyoweza kutengeneza kombinesheni bora kabisa katika klabu hiyo na
Serie A kwa ujumla kwa namna alivyoweza kushirikiana na viungo bora kabisa
waliowahi kuichezea klabu ya Udinese si wengine bali ni Gaetano D’Agostino na Gokhan
Inler.
Ni mchezaji mdogo kiumri na hakika
mategemeo ni mengi sana kwa mashabiki wa Juventus kwa huyu kijana Kwado
Asamoah.Ingawa angalizo kwa mashabiki na wadau wa klabu hiyo ni kuwa Asamoah
anahitaji muda ili kuweza kuzoea mazingira vyema ya uwanja(Juventus Areana) au
viunga vya mazoezi vya klabu hiyo vinavyojulikana kama Juventus centre.Akipewa
nafasi na kuaminiwa,Asamoah ataendelea kuifanyia Juve mambo makubwa kama yale
tulioyaona katika mechi dhidi ya Napoli katika lile pambano la Supercoppa
Italiana pale Beijing China.
Kila la kheri Kwado Asamoah katika maisha uliyoanza kunako
klabu ya Juventus.
0 comments:
Post a Comment