Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama the
three Lions Roy Hugson ameonyesha wasiwasi wake na uwanja wa Zimbru uwanja wa
nyumbani wa Moldova. Uwanja wa Zimbru ndio uwanja wa nyumabini wa Moldova
utakapofanyika mchezo wa kufuzu kombe la dunia baina yake na Uingereza siku ya
ijumaa.Hogson na kikosi chake wameamua kusafiri mapema kwenda Moldova ili
wakapate nafasi ya angalau kufanya mazoezi ili wasije wakashangazwa siku ya
mchezo.Uwanja wa Zimbru inasemekana ni mdogo na majukwaa yake yapo karibu na
uwanja wa kuchezea na wanasema kiwango hiki sio cha ligi kuu labda ligi daraja
la pili maarufu kama( Champioship). Hata beki wa kutumainiwa wa Uingereza pamoja na Chelsea Gary Cahill
“anasema sehemu yenyewe inaahidi na kuonyesha kabisa sio nzuri na ndio maana
tumesafiri mapema kuzoea uwanja”
Hogson anasema kuna mambo kibao ya kutegemea unapoenda
sehemu na nchi kama Moldova anasema unaweza ukajiuliza maswali kama je uwanja utakuwaje?au je hali ya hewa
kwa ujulma itakuwaje? au je vipi sehemu wenyewe ya kuchezea na vipi kuhusu ina
ya wachezaji unaoenda kukutana nao? kwa hiyo lazima pia tuangalie wachezaji
waliopo na jinsi gani tinajiandaa na kwa
ujumla kuna mambo mengi ya kuangalia kuelekea mchezo wenyewe.Anasema najua
katika kikosi changu kuna mawazo kibao kuhusiana na timiu tunayoenda kukutana
nayo na wengine watasema sio timu ya kutisha lakini hatuwezi kwenda kwenye
mchezo huo na mawazo kama hayo lazima tuwe makini sana.
Lazima twende huku tukijua fika kwamba Moldova sio timu ya
kubeza kwani michezo yao ya mwisho ya kufuzu walitoa sare na kufungwa tena kwa
ushindi mwembamba dhidi ya Uholanzi.
0 comments:
Post a Comment