
Ligi Kuu ya soka nchini Ujerumani (Bundesliga) iliendelea jana ambapo kulikwa na pambano zuri na la kusisimua kati ya Augusburg dhidi ya VFL Wolfsburg ikiwa ni raundi ya tatu ya Ligi hiyo.Mechi nyingine zitachezwa leo ambao kutakuwa mechi kadha wa kadha lakini mechi kubwa inayotarajiwa kutazamwa na wapenzi wengi wa soka ni mechi kati ya mabingwa watetezi Borrusia Dortmund dhidi ya Bayer 04 Levekursen pambano likipigwa pale Signal Iduna Park.Watu wengi wanalitazama pambano hilo kwa umakini mkubwa kwani litakuwa na mgeni rasmi ambaye ni Kansela wa Ujerumani Dokta Angela Merkel.Kansela huyo aliyekuwa katika uzinduzi wa kampeni ya fursa sawa kwa wote likilenga wale wahamiaji ambao wanakadiriwa kuwa milioni 16 nchini Ujerumani na upingaji wa ubaguzi wa rangi atakuwa shuhuda wa pambano la Dortmund dhidi ya Leverkusen pale katika jiji la Dormund.Kampeni hiyo imebatizwa jina la "Geh' Deinen Weg" kwa maana ya fursa sawa kwa watu wote hasa katika huduma za jamii kama elimu,afya na kuhamasisha amani katika nchi ya Ujerumani.Timu zote za Bundesliga 18 zitabeba maandishi hayo "Geh' Deinen Weg" ikiwa ni kampeni maalum kwa mechi zote za Ligi Kuu ya soka nchini Ujerumani katika raundi ya tatu iliyoanza jana 14/09 mpaka siku ya Jumapili tarehe 16/09/2012.Kabla ya kushuhudia pambano hilo la Dortmund na Leverkusen,Kansela Angela Merkel atakutana na vijana wanaolelewa na vilabu hivyo katika shule za soka na kuzungumza nao mambo mbalimbali ya kijamii na baadaye kushuhudia pambano hilo la kukata na shoka baina ya vilabu hivyo vikubwa nchini Ujerumani.Kampeni hiyo inasimamiwa na mfuko wa jamii hapo nchini Ujerumani unaoitwa 'the German Integration Foundation' ambao upo chini ya usimamizi wa Kansela Angela Melkel.
Vikosi vya timu zote mbili ni hivi hapa.
Borussia Dortmund: Weidenfeller - Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer - Gündogan, Kehl - Blaszczykowski, Reus, Großkreutz - Lewandowski
Bayer 04 Leverkusen: Leno - Carvajal, Wollscheid, Toprak, Kadlec - L. Bender, Reinartz, Rolfes - Castro, Kießling, Schürrle
0 comments:
Post a Comment