Zlatan IBRAHIMOVIC

- Nationality :
Swedish
- Age :
- 30 years
- Date of birth: :
- 3 October 1981
- Height :
- 1.95 m
- Weight :
- 95 kg
- Number :
- 18
- Position :
- Forward
- Club :
- PSG
- Kocha wa zamani wa klabu ya Inter Milan Jose Mourinho alimpa jina la Ibra Cadabra kwa maana ya mwanamazingaombwe kutokana na uwezo wake wa kufunga magoli kwa staili tofauti tofauti.Kwa wale wapenzi wenzangu wa Serie A watakubaliana nami kuwa tumempoteza nyota katika Ligi hiyo ya nchini Italia.Zlatan si mgeni katika masikio ya wengi kwani tangu dunia ianze kumtambua akiwa na klabu ya Ajax Amsterdam katika miaka ya 90,na baadaye kuvichezea vilabu kama Juventus,Inter,Barcelona na badaye AC Milan,Zlatan Ibrahimovic bado ameendeleza moto wake katika Ligi Kuu ya soka nchini Ufaransa maarufu kama 'French Ligue 1' akiwa na klabu ya PSG.Tayari amekwishafunga magoli 5 mpaka sasa na akiongoza kwa ufungaji katika Ligi hiyo ya Ufaransa.Zlatan Ibrahimovic ameshacheza dakika 360 mpaka sasa zikiwepo dakika 90 za mechi ya jana Ijumaa 14/09/2012 dhidi ya timu ya Tolouse iliyo chini ya kocha Casanova.Klabu hiyo ya Tolouse ilikubali kichapo cha magoli 2 kwa bila mbele ya PSG.Magoli ya PSG yalifungwa na Zlatan Ibrahimovic pamoja na Javier Pastore.
0 comments:
Post a Comment