

Klabu ya soka ya ASO Chlef ya nchini Algeria iliwashangaza mabingwa watetezi wa klabu bingwa bararni Afrika klabu ya Esperance Sportive Tunis ya nchini Tunisia mara baada ya kuifunga timu hiyo kwa goli moja kwa bila katika mwendelezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.Ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa klabu hiyo ya Esperance kupoteza katika hatua ya makundi katika mechi nne zilizokwishakuchezwa na hivyo kuweka tahadhari katika michuano hiyo kuwa bingwa anaweza kuwa yoyote kwa sababu timu zote zimeonesha kujiandaa vyema.Goli la ASO Chlef lilifungwa na mchezaji Anicet Eyenga katika pambano lililopigwa uwanja wa Mohamed Boumezrag unaomilikiwa na klabu ya Chlef.
Katika hatua nyingine,Ligi hiyo ya Mabingwa Barani Afrika inatarajiwa kuendelea kesho Jumapili(16/09/2012) ambapo kutakuwa na mechi mbili.Mabingwa wa zamani wa Kombe hilo timu ya TP Mazembe wakuwa wageni wa Belkum Chelsea pale Ghana na mechi nyingine ikiwa ya watani wa jadi katika nchi ya Misri ambapo klabu ya AL Ahly itawakaribisha Zamalek katika ile' Cairo Derby'.
0 comments:
Post a Comment