Ni raundi ya nne ya mwendelezo wa Ligi Kuu ya soka nchini Uingereza maarufu kama 'Barclays Premier League au EPL'.Kukiwa na mechi takribani tisa kwa siku ya kesho(Jumamosi) na moja kati ya mechi hizo tisa ni mechi ya Queens Park Rangers(QPR) dhidi ya Chelsea.Ni mechi inayosubiriwa kwa hamu sana na wapenzi wengi wa kabumbu kwani inatazamwa kama mechi iliyojaa purukushani na ushindani mkubwa kwa kuwa nje ya uwanja na ndani ya uwanja baadhi ya wachezaji wa vilabu hivyo wamekuwa na chuki za hapa na pale na hivyo kupelekea kuwa na uhasama wa moja kwa moja kutokana na kuwepo kwa chembechembe za ubaguzi wa rangi.Moja kwa moja nawazungumzia wachezaji Anton Ferdinand wa QPR na John Terry wa Chelsea.Vita ya wachezaji hawa ilianza tangu msimu uliopita katika pambano la mahasimu hao wa jiji la London nchini Uingereza katika uwanja wa Loftus Road unaomilikiwa na klabu ya QPR.Lakini jambo lingine lililojitokeza ni kuwa uhasama wa wachezaji hao umeamia mpaka kwa wachezaji wengine ambao ni Rio Ferdinand ambaye ni kaka wa Anton Ferdinand pamoja na Ashley Cole.Vita ya Rio na Ashley Cole imekuja wakati ambapo Ashley alimtetea nahodha wake wa Chelsea John Terry kuwa hakufanya kitendo chochote cha ubaguzi wa rangi jambo ambalo liliibua uhasama kati ya Rio na Cole ambapo Rio alichukizwa na Cole kumtetea Terry katika kesi ya ubaguzi wa rangi iliyokuwa ikimkabili Terry.Katika kesi hiyo Terry hakuonekana na hatia na hivyo kuachiwa huru.
Swali lakujiuliza baada ya mkasa huo wa msimu uliopita ni kuwa Je,Anton Ferdinand atamshika mkono John Terry katika pambano la kesho pale Loftus Road?Tusubiri tuone
0 comments:
Post a Comment