
Ni siku iliyokuwa imejaa matukio mengi ambayo kila mtu na
kila shabiki yalimsisimua na hakika ilikuwa ni mechi ilyokutanisha wanaume
kweli kweli.Achilia mbali mpambano wa wachezaji uwanjani ni vita kweli kweli
lakini pia sikiliza nyimbo na mapambio ya mashabiki wa timu zote mbili hii
inatokea mara chache sana katika msimu.Matukio yaliyojawa na hisia kali pamoja
na uhasama yalikuwa ni mengi lakini yote kwa yote hatimaye Patrice Evra
amekubali kushikana mkono na Luis Suarez.Tukio hili lilishidikana kwa takribani
miezi 7 iliyopita lakini tukio la Hillsborough limemgusa kila mtu na Evra” anasema
ilikuwa ni vizuri kusahau nyuma tofauti zetu na kupisha umuhimu wa siku
yenyewe”.

Anaendelea anasema ilikuwa ni mechi kubwa baina timu timu
kubwa na kitu muhimu ilikuwa kuonyesha heshima kwa mashabiki waliopo na wale
waliotutoka.Kulikuwa na janga kubwa katika historia ya klabu lakini watu
walikuwa wanaongelea suala la kushikana mikono ambalo mimi sioni kama ni muhimu
zaidi ya historia ya klabu.Evra anasema yote kwa yote nimefurahi sana kwasababu
amenishika mkono na kuonyesha kwamba wote tunaziheshimu familia zilizopoteza
jamaa zao na ilikuwa ni siku ngumu sana.
0 comments:
Post a Comment