
Baada ya kucheza michezo mitano bila ya ushindi katika mchezo mmoja yule bundi naona bado anaendelea kuindama klabu ya Liverpool kwani baada ya kipigo cha jana Anfield dhidi ya mashetani wekundu Manchester United wamepokea taarifa ya uwezekano wa kumkosa beki wao wa pembeni Martin Kelly kwa msimu mzima wa ligi uliobaki.Katika mchezo ambao Liverpool wealidhamilia kuandika ushindi wao kwanza msimu huu na pengine kuwa kama zawadi katika tukio la kuwakumbuka mashabiki wao takribani 96 waliopotea kule Hillsborough lakini ikawa moja kati ya zile siku ambazo hazikuwa tena nzuri kwao.Martin Kelly anatarajia kufanyiwa upasuaji katika sehemu yake ya goti mguu wa kulia na bado kocha Brendan Rodgers anasubiri maendeleo ya beki Daniel Agger.
0 comments:
Post a Comment