Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Monday, September 10, 2012

DAVID HAYE: VITALI KWANGU HAFIKI HATA RAUNDI YA SITA


 
Maneno haya yanamtoka Muingereza David Haye baada ya kushuhudia Vital Klitschko akimchakaza kwa kumchanana vibaya  juu ya jicho Mjerumani Mannuel Charr raundi ya pili  katika uwanja wa olympic Arena jijini Moscow. David Haye  anasema Vitali mwenye umri wa miaka 41 kaka wa Wladimir Klitschko japo ameshinda lakini nimeona mapungufu mengi kwenye kuzuia ama kujilindana na kama akikutuna na mimi nina uhakika hawezi kuvuka hata raundi ya sita.Nimesikitishwa sana na kiwango cha Vitali na ningependa kupambana naye na kummaliza.Anaendelea anasema Vitali ni mpiganaji lakini nina uhakika nitakopomrushia makonde hawezi kuyazuia na hakika leo hakucheza vizuri na amejiaibisha mwenyewe.

David Haye baaada ya kusamehewa adhabu yake ya kufungiwa  baada ya kuleta vurugu mwezi wa pili pale Darek Chisora aliposhindwa kwa pointi na Vitali analitafuta pambano na Vitali kwa nguvu zote hasa baada ya mwaka jana kupigwa na Mdogo wake Wladimir Klitschko na hivyo anafuta nafasi ya kulipiza kisasi.Haye anasema pambano lake na Vitali ana uhakika sio tu kwamba litakuwa kali na lakusisimua lakini pia litakuwa pambano bora katika historia ya masumbwi duniani hasa kutokana na ukweli kwamba amerudi katika ubora wake baada ya kumshinda Chisora mwezi wa saba. Pambano kati ya David Haye  na Vitali Klitschko ni pambano ambalo linasubiriwa kwa hamu katika ulimwengu wa masumbwi duiniani  na linatarajiwa kufanyika mwezi wa pili mwakani lakini likitegemea zaidi kama Vitali atashindwa katika kinyanga’nyiro cha kuingia Bungeni nchini Ukraine.

0 comments:

Post a Comment