Unaweza ukasema chochote lakini Habari hizi ni bundi ambaye
ameanza kulia kwenye nyumba ambayo ndio kwanza imenza kusahau habari za
misiba.Habari hizi sio mbaya kwa Abou Diaby peke yake bali pia Arsene na
Arsenal kwa ujumla kwani ndo kwanza
amerudi kutoka majeruhi akiwapa ushindi Arsenal na Ufaransa kwa pamoja.Abou
amepata tatizo la msuli mdogo na hii inamaanisha anaweza akakosa mchezo wa
nyumbani wa Ufaransa dhidi ya Belarus na
pia mechi ya ligi kuu ya premier dhidi ya Southampton kwenye dimba la Emirates.
Habari hizi zinakuja wakati ambao Didier Deschamps amesifia
uwezo wa Diaby akiwa amefunga goli pekee katika ushindi wa Ufaransa dhidi ya
Finland katika kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia nchini Brazil akisema ni kiungo ambaye amekamilika.Akieleza majeraha hayo kocha wa
Ufaransa Deschamps anasema amepata maumivu mabaya ambayo yanamfanya asitembee kwa uhuru na leo hatutamruhusu kufanya
mazoezi.Anaendelea anasema sio yeye tu hata Gael Clichy watapata wakati mgumu
kuweza kuwahi mechi dhidi ya Belarus.
0 comments:
Post a Comment