Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Sunday, September 9, 2012

ABOU DIABY:ILIANDIKWA NITARUDI



Bahati ni kitu ambacho kila mwanadamu anaomba kukutana nacho kwenye kila wazalo au afanyalo hata kama ana uwezo kiasi gani. Japo kwa kiasi kikubwa maandalizi yanatakiwa yakutane na fursa ili kutengeneza bahati lakini  wakati mwingine hivi vyote vinakuwepo lakini bahati inakosekana na hili linapotokea moja kwa moja binadamu hukata tama.Na hili ndilo lilimkuta Abou Diaby kwa sabubu maandalizi alikuwa nayo na fursa ya kucheza alikuwa nayo lakini anakosa bahati ya kuyaepuka majeraha na mwisho hafanyi kile anachokusudia.Hata Lionel Messi , Cristiano Ronaldo wanaihitaji sana hii neema ili waendelee kuwa na ubora walionao kwa sasa.

Abou Diaby amepitia kipindi kigumu sana katika maisha yake ya soka akiandamwa sana na majeruhi.Nakumbuka pambano fulani pale Emirates Arsenal wanacheza dhidi ya Newcastle United alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya Joe Barton kumchezea vibaya lakini yeye aligeuka David Haye.Lakini unaweza kuwa kwenye akili ya Diaby kwamba sio tu alikuwa anawaza kurudi tena kwenye kitanda cha matibabu lakini pia nina imani alimwita Joe Barton mshirikina kama sio mchawi maana alionekana kabisa alijua alichokuwa anakifanya.

Lakini Diaby sasa amerejea na amenza kuonyesha kile watu walichokuwa wanakitegemea toka kwake kwa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa. Na anasema huu ni msimu  muhimu sana kwangu nafanya kazi kubwa sana kuweza kupata mafanikio kuliko wakati mwingine wowote na nataka kumuonyesha kila mtu kwamba ninaweza.Nimefikia umri na wakati katika maisha yangu ya soka kuuonyesha uwezo wangu kwa muda mrefu na kusahau kila kitu nyuma na hakika iliandikwa nitarejea na wakati wa kuifanyia makubwa Arsenal ni sasa kama sio sitaweza tena.

Uwezo alionyesha kwenye mechi dhidi ya Liverpool sio tu kwamba uliipa Arsenal ushindi wa kwanza kwa msimu huu lakini pia alipata tuzo ya mchezaji bora wa mchezo na hatimaye kurudishwa katika timu ya taifa ya Ufaransa.Katika mchezo huo Diaby alifunga goli pekee dhidi ya Finland  kuwania kufuzu fainali za  kombe la dunia zitakozfanyika nchini Brazil 2014.Kocha wa Ufaransa wa sasa Didier Deschamps naye hakubaki nyuma kumsifia Diaby anasema sio tu kwamba ni kiungo mwenye kila ubora lakini pia nafahamu  kwamba ni kiungo aliyekamirika. Naye kiungo mwenzake  Rio Mavuba anasema pengo lake kwenye kikosi ni vigumu kuliziba emethibitisha tena ubora wake na ameweza kizibiti presha ya mchezo na nina imani ataendelea hivyo.





0 comments:

Post a Comment