Southampton au 'the Saints' au
watakatifu kwa kikwetu hakika wanaonekana hawakuja na kuondoka bali wataishi
milele.Wakirudi daraja la premier la ligi kuu nchini Uingereza baada ya miaka
saba hakika ulikuwa ni ukaribisho mzuri kwao kukutana na watetezi wa taji
matajiri wa jiji la Manchester au wanapenda kujiita 'the Citizen' au kikwetu
wananchi ama raia.Kikubwa kilchonifurahisha kwenye mechi hii ni jinsi
watakatifu walivyokuwa sio waoga, walivyokuwa wanafunguka na jinsi
walivyokuwa wanashuka na kujenga mashambulizi yao ya
kushtukiza(counter attacks) ambayo yalikuwa ya kujiamini sana.Kumbuka walikuwa
Etihadi uwanja ambao City wana rekodi ya kutopoteza michezo 30 wakishinda 28 na
msimu uliopita wakifungwa magoli 12 tu chini ya nahodha Vicent Company lakini watakatifu
wakafunga mabao mawili.
Natamani sana kuwaona watakatifu
wakicheza kwenye ligi yao kwa maana ya kuchea na vilabu vya daraja lao vilabu
ya kariba ya Swansea,QPR,Norwich,Wigan,Aston Villa,Stoke City,Reading na
West Ham.Kocha Adkins alionyesha kwamba ana watu ambao wanaweza kuipa
shida beki ya timu yoyote atakayokutana nayo.Akianza kwa kumuacha benchi
Rickie Lambert na kuanza na Jay Lodriguez kutoka Bunrey ambaye ni usajili pekee
walioufanya mara tu baada ya kupanda daraja bado watakatifu walionekana
hatari pale Etihad.Rickie Lambert mfungaji bora wa ligi daraja la pili
(championship) msimu uliopita na pia tayari akiwa ameshawafungia watakatifu
mabao 88 katika michezo 158 ilimchukua dakika 4 tu kufungua akaunti yake ya
magoli katika ligi kuu nchini Uingereza na pengine kuwemo katika orodha ya
wafungaji bora msimu huu akiwa na miaka yake 30.
Japo City ushindi wao katika
mechi tatu zilizopita wameupata huku wakikaribia kupoteza mchezo lakini
goli la Rickie Lambert lilifanya matokeo kuwa 2 -1 na kuwafanya watakatifu
wahisi sio tu kupata point za kwanza bali pia kuvunja rekodi ya Etihadi kabla
ya Nasri na Dzeko kufanya matokeo kuwa 3-2 wakitanguliwa na Tevez .Uelewano
wa Carlos Tevez na Kun Agguero hasa katika mechi sita za mwisho msimu uliopita
zingetosha kuitisha ngome ya timu yoyote.Hata hivyo Robert Mancini
hakuhitaji mguu wa Agguero uliompatia kombe msimu uliopita ili kufungua mvinyo
kwani aliumia mapema safari hii alihitaji zaidi filimbi ya mwisho ya Howard Webb
manake watakatifu walikuwa wanakuja kila
dakika.
Kwa Southampton kikubwa
kilichokuwa kinawazuia kurudi kwao misimu saba iliyopita ni kuuzwa kwa baadhi
ya nyota wake ambao walionekana ni wakubwa kuliko watakatifu. Unakumbuka
nyota kama kina Bale,Theo Walcott pamoja Alex-Oxlade Chamberlain lakini
Adkins ndani ya misimu mitatu amefanya kazi kubwa kuwatoa daraja la tatu mpaka
ligi kuu kitu ambacho sio tu kimeirudisha premier league pale St.Marry's bali
pia ameweza kulinda kazi yake kama kocha na kazi kubwa iliyobaki ni kuhakikisha
wanabaki na wanaishi milele
MECHI ZINAZOFUATA.
Liverpool Vs Manchester City Anfield
Southampton Vs Wigan St Marry's
0 comments:
Post a Comment