Southampton au 'the Saints' au watakatifu kwa kikwetu hakika wanaonekana hawakuja na kuondoka bali wataishi milele.Wakirudi daraja la premier la ligi kuu nchini Uingereza baada ya miaka saba hakika ulikuwa ni ukaribisho mzuri kwao kukutana na watetezi wa taji matajiri wa jiji la Manchester au wanapenda kujiita 'the Citizen' au kikwetu wananchi ama raia.Kikubwa kilchonifurahisha kwenye mechi hii ni jinsi watakatifu walivyokuwa sio waoga, walivyokuwa wanafunguka na jinsi walivyokuwa wanashuka na kujenga mashambulizi yao ya kushtukiza(counter attacks) ambayo yalikuwa ya kujiamini sana.Kumbuka walikuwa Etihadi uwanja ambao City wana rekodi ya kutopoteza michezo 30 wakishinda 28 na msimu uliopita wakifungwa magoli 12 tu chini ya nahodha Vicent Company lakini watakatifu wakafunga mabao mawili.
 |
Rickie Lambert |
|
Natamani sana kuwaona watakatifu wakicheza kwenye ligi yao kwa maana ya kuchea na vilabu vya daraja lao vilabu ya kariba ya Swansea,QPR,Norwich,Wigan,Aston Villa,Stoke City,Reading na West Ham.Kocha Adkins jana alionyesha kwamba ana watu ambao wanaweza kuipa shida beki ya timu yoyote atakayokutana nayo.Akianza jana kwa kumuacha benchi Rickie Lambert na kuanza na Jay Lodriguez kutoka Bunrey ambaye ni usajili pekee walioufanya mara tu baada ya kupanda daraja bado watakatifu walionekana hatari pale Etihad.Rickie Lambert mfungaji bora wa ligi daraja la pili (championship) msimu uliopita na pia tayari akiwa ameshawafungia watakatifu mabao 88 katika michezo 158 ilimchukua dakika 4 tu kufungua akaunti yake ya magoli katika ligi kuu nchini Uingereza na pengine kuwemo katika orodha ya wafungaji bora msimu huu akiwa na miaka yake 30.
 |
Theo Walcott |
Japo City ushindi wao katika mechi tatu zilizopita wameupata huku wakikaribia kupoteza mchezo lakini goli la Rickie Lambert lilifanya matokeo kuwa 2 -1 na kuwafanya watakatifu wahisi sio tu kupata point za kwanza bali pia kuvunja rekodi ya Etihadi kabla ya Nasri na Dzeko kufanya matokeo kuwa 3-2 wakitanguliwa na Tevez . Kuumia mapema kwa Kun Agguero ambaye katika mechi sita za mwisho msimu uliopita zilikuwa na uelewano mkubwa baina yake na Tevez na kuwapa kombe lakini jana Robert Mancini alihitaji zaidi filimbi ya mwisho ya Howard Webb ili kuweza kufungua mvinyo manake watakatifu walikuwa wanakuja tu.
Kwa Southampton kikubwa kilichokuwa kinawazuia kurudi kwao
misimu saba iliyopita ni kuuzwa kwa baadhi ya nyota wake ambao walionekana
ni wakubwa kuliko watakatifu. Unakumbuka nyota kama kina Bale,Theo
Walcott pamoja Alex-Oxlade Chamberlain lakini Adkins ndani ya
misimu mitatu amefanya kazi kubwa kuwatoa daraja la tatu mpaka ligi kuu
kitu ambacho sio tu kimeirudisha premier league pale St.Marry's bali pia
ameweza kulinda kazi yake kama kocha na kazi kubwa iliyobaki ni
kuhakikisha wanabaki na wanaishi milele
0 comments:
Post a Comment