Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Tuesday, August 21, 2012

MAROUANE FELLAINI AWAHARIBIA VAN PERSIE NA KAGAWA











Alikuwa ni  Marrouane Fellaini na mchezaji bora wa mchezo   wa jana aliyeharibu kabisa siku ya  Sir Alex na mashabiki wa Manchester Utd kote ulimwenguni baada ya goli lake kuipa Everton na mashabiki wote pale marseysides sio tu point tatu bali pia zawadi ya Idd.Inaweza kuwa mechi ya Manchester Utd na Everton ilyojaza mashabiki sio tu kwenye uwanja wa Goodson Park bali pia hata hapa nyumbani kwetu Tanzania kutokana na sababu kuu mbili.



 Kwanza kabisa ni mchezaji bora wa chama cha waandishi wa habari za michezo na pia mfungaji bora wa ligi kuu ya Premier nchini Uingereza msimu uliopita Robin Van Persie.Sio tu Sir Alex ambaye bado haamini mchezaji huyo kutoka Arsenal kutua Old trafford lakini pia hata mashabiki wenyewe nao bado kama hawaamini ami i hivi na wamekuja kuona kama sio kushuhudia akiendeleza mambo aliyoyafanya na arsenal msimu uliopita.Kama mchezaji mpya kikosini pamoja na Shinji Kagawa ingekuwa vema na faraja sana kwao kama wangeanza na ushindi.Lakini la pili ni kuona Utd wanaanza vipi ligi hasa baada ya wapinzani wao wakubwa kwenye taji msimu huu matajiri wa jiji au wananchi Manchester City kuanza na ushindi jana

KIUFUNDI
Manchester hawakuwa na mabeki wao wote wa kati na pembeni wakianza na Valencia kulia pamoja na Karrick katikati na kila mara inapotokea mpira wowote wa adhabu basi Nikica Jelavic na Marouane Fellaine walionekana hatari.Bado walikuwa wanapata shida kupata muunganiko mzuri wa Rooney ,Kagawa 
 na Wellbeck  pia Upande wa Patrick Evra ambao umekuwa na nguvu sana hapo nyuma unaoenekanakuzorota siku hadi siku .Hata Robin Vanpersie alipoingia kuchukua pahala pa Wellbeck alionekana labda kucheza nyuma ya mshambuliaji ndio kunakomfaa zaidi kuliko kucheza straika mkuu nafasi ambayo alicheza Arsenal msimu uliopita.

MECHI INAYOFUATA.
Baada ya kupoteza mchezo wa jana Manchester watakuwa Old Trafford Jumamosi wakiwakaribisha watoto wa Martin Jol Fulham ambao wamenza ligi vizuri.Baada ya Van Persie kuanzia bechi leo Sir Alex atakuwa na nafasi ya kumunzisha pamoja na Wayne Rooney ili waanze kutengeneza uelewano na kuanza biashara ya kufunga magoli.Everton kwa upande wao watakuwa Villa Park kuwakabili Aston Villa na watatamani kuendeleza wimbi la ushindi walioupata jana.

KUMBUKA
Katika historia ya ligi kuu nchini uingereza ni  timu moja tu ambayo mara mbili  imeweza kupoteza mchezo wa ufunguzi na kuja kuchukua ubingwa.Na timu hiyo ni machester Utd msimu wa 1992-1993 na 1995-1996 kwa hiyo mashabiki wa Utd hawapaswi kupoteza tabasamu kutokana na matokeo ya jana.

0 comments:

Post a Comment