Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Wednesday, August 29, 2012




 

 Usajili wa Luka Modric kutoka Tottenham Hotsupurs yawezekana umekuja wakati muafaka wakati Jose Mourinho na Real Madrid wakijiandaa na mechi ya Marudiano ya Supercup na FC Barcelona katika uwanja wa Santiago Bernabeu.Real Madrid bado wanahangaika kupata ushindi wao wa kwanza kwenye LaLiga na kwa hakika walikuwa wanahitaji huduma ya Mcoratia  huyu ili kuweza kumfukuza FC Barcelona.Baada ya kutoka sare ya 1-1 na Valencia na baadae kufungwa 2-1 na wapinzani  na majirani  zao Getafe Real Madrid wanakibarua kizito kusawazisha ushindi wa Fc Barecelona wa 3-2 walioupata pale Camp Nou.Baada ya mechi Jose Mourinho alikaririwa akisema" tulistahili kupoteza mchezo na hatuwezi kukubaliana na kuendelea kucheza mchezo wa jinsi hii" na kitu kikubwa kilichomkera Jose Mourinho ni magoli yaliotokana na mipira iliyokufa.Naye Cptain Iker Casilas anasema"kimsingi tunakubaliana na mwalimu kwamba tulicheza vibaya lakini kikibwa tunatakiwa kusahau kwani tuna mchezo muhimu mbele yetu wa El Clasico. Katika mchezo huu Jose Mourinho anaweza kuendelea bila huduma ya beki wake kipenzi Pepe mbaye pia alikosa mchezo uliopita pia Tunaweza kushuhudia Luka Modric akipata mechi yake ya kwana tangu amalize usajili juzi japo pia sio utaratibu wa Jose Mourinho au"The only one"

 Barecelona kwa upande wao kila kitu kinaonekana kumwendea vizuri kocha Ttto Vilanova kwani licha kuongoza msimamo wa La Liga lakini ana asilimia mia moja ya pointi zote lakini shukrani nyingi zimwendee mchezaji bora wa dunia Lionel Messi.Huku mpinzani wake Ronaldo gari lake likisusua yeye la kwake tayari linaonekana limechangamka.Lionel Messi tayari ameshafunga magoli 5 mpaka sasa kwenye mashindano yote akifunga kwa penati kwenye Supercup mechi  ya kwanza na wikiendi iliyopita wakionekana kama wanapoteza mchezo dhidi ya Osasuna Lionel Messi kafunga tena 2 na kuashiria sio tu Barcelona kuanza vizuri bali pia  Lionel Messi mwenyewe akianzia alipoishia msimu uliopita.Kocha Titto Vilanova anaweza kuwa na wasiwasi na nahodha wake Puyol baada ya kupata maumivu kwenye mechi na Osasuna lakini tunweza kushuhudia Alex Song akipata mechi yake ya kwanza baada ya kusajiliwa kutoka Arsenal.
























0 comments:

Post a Comment