Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Monday, August 20, 2012

TP MAZEMBE YAIFUNGA ZAMALEK HUKU SAMATTA AKIFUNGA GOLI LA USHINDI.

Klabu ya TP Mazembe jana ilijihakikishia nafasi ya kucheza nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuitoa katika mashindano timu ya Zamalek katika michezo ya kundi B ya Ligi hiyo.Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja unaomilikiwa na jeshi la Misri maarufu kama(Cairo Military Academy Stadium).Mabingwa hao wa Kombe hilo la Klabu bingwa Afrika katika miaka ya 2009 na 2010 wapo kundi moja na Al Ahly(Misri),Berekum Chelsea(Ghana) na Zamalek(Misri).
Berekum Chelsea
Magoli ya Mazembe yalifungwa na Mzambia Hichani Himoondena pamoja na Mtanzania Mbwana Samatta ambaye alifikisha magoli 5 katika michuano hiyo huku goli la Zamalek likifungwa na Razak Omotoyossi.

Berekum Chelsea dhidi ya Al Alhy
Wakati huo huo klabu ya Berekum Chelsea ililazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya timu ya Misri ya Al Ahly katika mchezo mwingine wa kundi B

0 comments:

Post a Comment