BRITANIA |
Hii ni moja kati ya zile mechi ambazo sio wachezaji tu bali pia hata mashabiki wa Arsenal hawazipendi sana lakini ni mechi ambayo inawapa nafasi ya kuonyesha msimu huu wamejiandaa kiasi gani.Achilia mbali aina soka wanayocheza na aina ya wachezaji waliyonayo lakini ni mechi ambayo inawakumbusha mashabiki wa Arsenal mwezi wa pili 2010 tukio baya la kuvunjika kwa Aaron Ramsey.Kocha wa Soke City Ton Pills anapenda sana kukutana na Arsenal na Arsene wenger kwa sababu anajua kwa aina yake ya soka inawapa shida na nadhani akishinda ndio anakuwa na raha kuliko siku nyingine yoyote ya msimu.
Pennant vs Song |
HABARI ZA TIMU.
STOKE CTY
Tukinza na wenyeji Stoke City hawana majeruhi wapya kuelekea katika mchezo huu japo hakika watamkosa Dean Whitehead ambaye anatumikia adhabu baada ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Reading. Stoke watamkaribisha mchezaji wa zamani wa Arsenal Jermaine Pennant ambaye alikosa mechi ya ufunguzi kwa majeraha pia Geoff Cameron atakuwepo baada ya kupokea kibali chake baada ya uhamisho wake toka Marekani.
KIKOSI CHAWEZA KUWA HIVI.
Begovic,Wilson,Wilkinson,Huth,Shawcross,Palacios,Whelan,Etherington,Kightly, Walters,Crouch.
ARSENAL.
Kwa upande wa Arsenal watamkaribisha Alex-Oxlade Chamberlain baada ya kukosa mechi ya ufunguzi kutokana na majeraha na amefanya vizuri kwenye mazoezi ijumaa hivyo naye anaweza kuanza.Majeruhi wa mda mrefu Wilshere ataendelea kukosekana pamoja na Tomas Rosicky ambaye alipata majeraha kwenye michuano ya EURO. Raulent Coscielny naye ataendelea kukosekana kutokana na majeraha ya paja na atampa nafasi nzuri Per Martesacker kuweza kutumia vizuri urefu wake kumkabil Crouch pamoja na mipira ya kurusha.Pia kuna wasiwasi kidogo kwa goli kipa Wojciech Szcezesny ila kama takosekana itakuwa nafasi nzuri kwa Lukasz Fabianski baada ya kupona mgongo.Upande wa kulia pia Sagna ataendelea kukosekana kutokana na majeraha na Jenkinson ataendelea kuwa ndio chaguo pekee upande wa kulia.
KIKOSI CHAWEZA KUWA HIVI:
Szcezeny,Jekinson, Gibbs,Vermaeleen, Martesacker,Arteta,Diaby,Carzola,Poldoski,Gervinho,Giroud
KIUFUNDI.
Britania sio sehemu nzuri ya kutembelea sio kwa Arsenal tu bali hata kwa timu nyingine kubwa za Premier Ligi ya Uingereza.Stoke city wamekuwa wakitumia vizuri uwanja wao wa nyumbani na imekuwa silaha yao kuendelea kubaki kwenye ligi na sasa wana rekodi ya kutofungwa michezo 7 na pia ukizingatia Peter Crouch amekuwa na rekodi nzuri ya kufunga akikutana na Arsenal.

0 comments:
Post a Comment