Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Saturday, August 18, 2012

STEVE CLARKE AWALIZA LIVERPOOL

Msimu uliopita alikuwa kocha msaidizi katika kikosi cha Liverpool chini ya meneja Kenny Daglish.Msimu huu yupo na klabu ya West Bromwich Albion ambapo leo aliishuhudia timu yake hiyo mpya ya ikiipa kichapo cha mbwa mwizi klabu yake ya zamani ya Liverpool.

Romelu Lukaku aanza mambo West Bromwich Albion afunga goli moja wakati W.B.A wakiwafunga Liverpool.

Mladen Petric na Michu wainogesha EPL
Ukiwa ni msimu wake wa kwanza wa EPL hatimaye mshambuliaji wa Fulham ameonesha kwa kiasi gani Fulham hawakupoteza fedha katika kumsajili.Katika mechi ya leo dhidi ya Norwich Mladen Petric alifunga magoli mawili katika dk za 42 na 54 na kutoa pasi moja ya goli kwa Kacaklinic katika dk ya 66.
Wakati Mladen Petric akifunga mara mbili kwa Fulham,ingizo jipya katika EPL msimu huu namzungumzia Michu akiichezea klabu ya Swansea naye alitupia mara mbili dhidi ya QPR katika dk ya 8 na 53 na pia akatoa pasi ya goli kwa Scott Sincrail dk ya 81.




0 comments:

Post a Comment