Ronaldo vs Alves |
Kipindi cha kwanza kilianza taratibu na Bacrelona kuwa na umilki wa mpira kiasi kikubwa kama kawaida yao na Real Madrid wakiwasubiri kwenye mashambulizi yam kushitukiza.Kipindi cha pili ndio tukaiona El Clasico iliyotufanya tulio wengi kulala saa 7.
Kipindi cha pili kilinza kwa Real Madrid kufungua Supercopa accounts kwa goli la kichwa la Christiaono Ronaldo kabla ya Pedro ya kusawazisha mara tu mpira ulipoanza.Lionel Messi akafunga kwa penati baada ya Andres Iniesta na mchezji bora wa mchezo kufanyiwa madhambi na Sergio Ramos kabla ya Xavi Hernandez kufunga goli la tatu.Makosa ya kipa wa Barcelona Victor Valdez yakampa Angel Dimalia na Real Madrid goli la pili na kuifanya mechi ya pili ya marudiano pale Bernabeu iwe fainali kweli kweli.
TULIYOJIFUNZA.
Kwanza kabisa japo Barcelona wamemiliki mpira kwa kiasi kikubwa lakini Lionel Messi hakufanya makubwa sana kama kawaida yake zaidi ya kufunga penati.
Christiano Ronaldo pia amekuwa mtulivu sana hakufanya makubwa kama tulivyotarajia hata pale timu yake ilpopata nafasi kidogo ya kumilki mpira japo naye alifunga goli kutokana na kona ya Ozil.
Tumejifunza kuwa Real Madrid inapocheza bila Pepe inakuwa na utulivu sana.
Tumejifunza pia kwamba japo kila golikipa anafanya makosa lakini Victor Valdez ameendelea kutonivutia langoni kwa kumzawadia goli Angel Dimalia.
Tumejifunza kwamba japo huu ni ushindi wa Barcelona wa 6 kwenye mechi 9 mfululizo za El Clasico lakini ushindi wa kwanza wa Titto Vilanova akiwa kama kocha mkuu wa Barcelona.
Pia tumejifunza pia kwamba japo Jose Mourinho na Real Madrid wana Alonso, Khedira, Ozil, bado wanahitaji sana kumalizana na Tottenham hotspurs ili kumpata Luka Modric atamsaidia sana hasa katika mechi kama hii kutokana na uwezo wake kukaba na kushambulia.
MATOKEO YA EL CLASICO 2011-2012.
10 August: Spanish Super Cup, first leg - Real Madrid 2-2 Barcelona
17 August: Spanish Super Cup, second leg - Barcelona 3-2 Real Madrid
10 December: La Liga - Real Madrid 1-3 Barcelona
18 January: Spanish Cup, quarter-final, first leg - Real Madrid 1-2 Barcelona
25 January: Spanish Cup, quarter-final, second leg - Barcelona 2-2 Real Madrid
21 April: La Liga - Barcelona 1-2 Real Madrid
VIKOSI.
Barcelona. Valdez,Alves,Adriano,Mascherano,Pique,Busquet,Xavi,Iniesta,Sanchez,Messi.
Real Madrid. Casilas,Arbeloa,Contrao,Arbiol,Ramos,Alonso,Khedira,Ozil,Carlejon,Ronaldo,Benzema.
0 comments:
Post a Comment