Leo ni Ufunguzi wa Bundesliga na ni msimu wa 50 tangu ligi hiyo kuu nchini ujerumani kuanzishwa mwaka 1963. Katika Ufunguzi wa Bundesliga inwakutanisha mabingwa watetezi Borrusia Dortimund na Werder Bremen katika Uwanja wa Signal Iguna Park.
Borrusia Dortimund:
Kocha Juggen Klopp atapenda vijana wake sio tu waanze ligi pale atapenda kuweka historia ya timu ya kwanza kutwaa Bundesliga mara 3 mfululizo yaani( hat-trik).Borrisia Dortimund wamekuwa bize sana kwenye soko la usajili wakisajili na wakiuza baadhi y awachezaji. Lakini kikubwa ni kuondoka kwa shinji Kagawa aliyesajiliwa na Manchester United na kusajiliwa kwa mchezaji bora wa Bundesliga msimu wa 2011-2012 Marco Reus kutoka Borrusia Monchengladbach.
Werder Bremen:
Kocha mkongwe Thomas Schaafs atakuwa na kibarua kigumu mbele ya zadi ya mashabiki 83000 pale Sigal Iduna Park ukizangatia Bremen hawajashinda mechi 9 za mwisho msimu uliopita na bado hata maandalizi msimu huu si mazuri wakifunngwa kwen DFB Cup na timu daraja la tatu ya Breuben Munster 4-2. Bremen nao wamekuwa bize sana kwenye dirisha la usajili wakipoteza wachezaji wao nyota Claudio Pizzaro na Marko Marin kwa Bayern Muinch na Chelsea kwa pamoja hakika leo watakuwa na kibarua kizito.japo nao wamefanya usajili wa watu kama Arjelo Elia kutoka Juventus, Park na Theodor Gebre Selassie.
0 comments:
Post a Comment