Kama ilivyo ada ya tamthilia nyingi itakuwa ndefu na hata katikati kukuchanganya sana lakini sisi wafuatiliaji wazoefu tunajua tu mwisho lazima Ina atamuoa Angello,lazima Barbarita ataoana na Alejandro na hata tamthilia hii jina lake unalo tulijua tu kwamba Modric na Real Madrid lazima wataoana.Totteham wametangaza katika mtandao wao kwamba wamekubaliana na Real Madrid kumuuza Luka Modric kwa ada ya £30m lakini kikubwa ni kusaini mkataba wa ushirikiano baina ya hizo timu mbili.Luka Modric amesaini mkataba wa miaka mitano na baada ya kupimwa afya anatarajiwa kutangazwa mbele ya mashabiki wa Real Madrid Santiago Bernabeu katika mechi ya marudiano ya Supercup dhidi ya Barcelona.
Monday, August 27, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment