Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Monday, January 14, 2013

AFCON INASABABISHA MATATIZO KATIKA VILABU VINGI ULAYA


 

Makocha pamoja na mameneja wengi sana wanalalamika kuwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika maaarufu kama(AFCON) imekuwa ikisababisha vilabu vingi Ulaya na nje ya Ulaya kukosa wachezaji wake nyota ambao huondoka na kujiunga na nchi zao kwa ajili ya michuano hiyo.Mwaka huu michuano hii inafanyika nchni Afrika Kusini na kutakuwa na jumla ya wachezaji 368 toka vilabu mbalimbali katika mataifa 55 duniani.Hii ina maanisha kuwa wachezaji wengi wa Kiafrika wapo sehemu mbalimbali duniani wakicheza Ligi mbalimbali.

Katika nchi hizo 55 zipo nchi 27 za Ulaya zikiwepo nchi za Liechtenstein na Luxembourg bila kuvisahau vilabu toka Brazil,China na Marekani.Ligi ya Ufaransa siku zote hutoa wachezaji wengi katika michuano hii ya Mataifa ya Afrika na safari hii imetoa wachezaji 50 huku 15 wakitoka katika Ligi Kuu ya nchi hiyo maarufu kama (Ligue 1) ambao watakosa wiki tatu za michezo hiyo ya mataifa ya Afrika.

Kuna wachezaji 15 toka Ligi kuu ya soka nchini England,14 toka Ligi kuu ya soka nchini Ureno,10 kutoka La Liga ya nchini Hispania na sita kutoka Ligi kuu ya soka nchini Italia(Serie A).FIFA waliweka sheria ya kuvibana vilabu kuwaruhusu wachezaji wao kujiunga na kambi za timu zao za taifa siku 14 kabla ya mashindano.Klabu itakayoathilika na michuano hiyo ni klabu ya AJ Ajaccio ambayo itapoteza wachezaji 5 watakaoenda katika michuano hiyo na mpaka sasa klabu hiyo inakamata nafasi za chini katika Ligi kuu ya soka nchini Ufaransa maarufu kama (French Ligue 1).

Wachezaji walioamua kubaki na vilabu vyao na kuacha kujiunga na timu zao za taifa ni pamoja na Steven Pienaar na beki wa timu ya tifa ya visiwa vya Cape Verde Ricardo.

0 comments:

Post a Comment