Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Wednesday, November 7, 2012

UCL: CHELSEA YALIPIZA KISASI KWA SHAKHTAR

wachezaji wa Chelsea Mata na Cahill wakimpongeza Moses

Klabu ya Chelsea jana ililipiza kisasi katika michuano ya Klabu Bingwa  Ulaya mara baada ya kuifunga timu ya Shakhtar Donestic  toka nchini Ukraine.Ilikuwa ni mechi ya marudiano mara baada ya Chelsea kukubali kipigo cha magoli 2-1 katika mechi ya kwanza iliyofanyika uwanja wa Donbass Arena kunako nchi ya Ukraine.Katika mechi ya jana Chelsea iliibuka na ushindi wa magoli 3-2 kwa magoli ya Fernando Torre dk 6,Oscar dakika ya 40 na Victor Moses 90 huku magoli ya Shakhtar yakifungwa na William yote mawili katika dakika za 9 na 47.

0 comments:

Post a Comment