Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Friday, November 9, 2012

JE NI AL HILAL NA EL MERREIKH FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO?

Kwa mara ya kwanza klabu za ukanda wa kusini mwa Afrika na hasa toka nchi ya Sudan zinaweza kukutana katika fainali ya kombe la shirikisho kutokana na kuibuka na matokeo mazuri katika mechi za nusu fainali za kwanza dhidi ya FC Leopards ya Congo na Djoliba ya nchini Mali.Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa historia ya kombe hilo  kwa klabu mbili toka nchini moja kucheza fainali ya kombe hilo la shirikisho.

Miaka minne iliyopita ni timu za Tunisia zilicheza fainali ya kombe hilo na kabla ya hapo timu za Ghana nazo zilicheza katika fainali ya kombe hilo.Al Hilal iliifunga timu ya Djoliba ya nchini Mali kwa magoli 2-0 kwa magoli ya nyota toka nchi ya Senegal Ibrahim Sane na Msudani Mudhasir Eltaib wakati Al Merreikh iliifunga timu ya FC Leopards toka nchini Congo kwa magoli 2-1.

Je,hilo litatokea?tusubiri tuone

0 comments:

Post a Comment