Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Thursday, October 11, 2012

YANGA YAICHAPA TOTO JIJINI MWANZA



Timu ya Young Africans imeichapa 3-1 Toto Africans katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanznaia bara, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 
Mchezo ulianza kwa kasi mwanzo mwa mchezo tu kwa Yanga kufanya shambulizi langoni mwa wenyeji timu ya Toto Africans ambapo walinzi wa timuya Toto waliondoa hatari hiyo langoni mwao.



Dakika ya pili ya mchezo, mshambuliaji Didier Kavumbagu aliipatia Yanga bao la kwanza, baada ya jitihada binafsi za kumalizia mpira ambao aliupiga na kuokolewa na mlinda mlango wa Toto kabla ya Didider mwenye kumalizia na kuhasabu bao la kwanza.
 
Yanga ambayo iliingia uwanjani leo kwa lengo la kusaka point 3 muhimu, ilicheza kwa kuelewana sana kiasi kwamba wapenzi na washabiki waliojitokeza uwanja wa CCM Kirumba walifurahia soka hilo na kujikuta wakiwapigia makofi wachezaji wa Yanga kadri muda ulivyokua unakwenda.
 
Mbuyu Twite aliipatia Yanga bao la pili dakika ya 21 ya mchezo, kufuatia kupanda kwenda kuongeza nguvu ya mashambulizi, na kufanikiwa kuifungia timu yake bao la pilii baada ya uzembe wa walinzi wa Toto waliozembea kuondoa hatai langoni mwao.
 
Viungo wa Yanga, Niyonzima, Chuji, Domayo na Nurdin ambaye leo alirejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi kwa kipindi cha miezi 3 waliweza kutawala sehemu ya katikati na kuwapoteza kabisa wachezaji wa timu ya Toto African.
 
Mpaka mpira unakwenda mapumziko, wenyeji Toto Africans 0 - 2 Yanga
 
Kipindi cha pili, kilianza kwa timu ya Toto kutaka kusaka bao la mapema, lakini ukuta wa Yanga uliokuwa unaongozwa na Twite, Cannavaro, Juma Abdul na Oscar Joshua ulikua makini kuokoa hatari hizo.
 
Dakika ya 55, Toto Africans walipata bao la kwanza kufuatia uzembe wa walinzi wa katikati kutegeana kuokoa mpira uliokuwa katika eneo lao na kufanya mshambuliaji wa Toto kuipatia bao la kwanza.
 
Kocha Ernie Brandts aliamua kufanya mabadiliko dakika ya 62, ya kuwatoa Athuman Idd na Frank Domayo na nafasi zao kuchukuliwa na Shamte Ally na Daavid Luhende, mabadiliko ambayo yaliongeza uhai kwa timu ya Yanga.
 
Jeryson Tegete aliipatia Yanga bao la tatu dakika ya 69, mara baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanya na Didier Kavumbagu aliyewatoka walinzi wa Toto African na kumpasia mfungaji.
 
Yanga iliendelea kulishambulia lango la Toto African na katika ya 85 ya mchezo, mwamuzi aliinyima Yanga penati ya wazi kufuatia walinzi wa timu ya Toto kuwafanyia madhambi Tegete na Didier ndani ya eneo la hatari.
 Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Yanga 3-1 Toto African.
 
Baada ya ushindi wa leo dhidi ya timu ya Toto Africans, Yanga inafikisha jumla ya alama 11 sawa na timu ya Kagera Sugar ya Kagera, na kutofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa, huku ikiwa imecheza michezo 7, imeshinda 3, sare 2 na kufungwa michezo 2 
 
Yanga itaondoka kesho alfajiri kurudi jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wake unafuata dhidi ya timu ya Ruvu Shooting tarehe 11.10.2012. 
 
Yanga: 1.Berko, 2.Juma, 3.Oscar, 4.Twite, 5.Nadir, 6.Chuji/Luhende, 7.Domayo,Shamte, 8.Niyonzima, 9.Didier, 10.Tegete, 11.Nurdin
Taarifa na Mtandao wa Yanga

0 comments:

Post a Comment