Kiungo wa kutumainiwa wa Arsenal na timu ya taifa ya
Uingereza Jack Wilshere amemweleza kocha
wake Arsene wenger kwamba baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi 15
sasa yuko tayari kupambana.Wilshere jana alicheza dhidi ya Chelsea kwa dakika
tisini kwa mara ya kwanza tangu aumie mwezi wa nane msimu uliopita huku Arsenal
wakipoteza mchezo huo kwa 2-0.Kumbuka mchezo wenyewe ulihusisha vikosi vya
chini ya umri wa miaka 21 lakini pia kwa nyakati tofauti makocha hutumia hata
wachezaji wao wazoefu hasa wanapotoka katika majeraha.Achilia mbali mchezo wa
jana Wilshere pia tayari ameshacheza kwa dakika 136 katika michezo dhdi ya Westbromwich
Albion pamoja na Reading na sasa anasema yuko tayari hata kuwavaa Norwich
jumamosi pale Carow Road.Lakini tayari Wenger alishasema wazi kwamba lazima
waende taratibu taratibu japo kipaji na uwezo wa Wilshere unaweza ukamtia
majaribuni kocha yeyote na kujikuta ukimtumia pasipo kupenda lakini yeye anasema
atayashinda.Jopo la madaktari na Wenger wamempamgia
mchezo mwingine wa kujipima nguvu dhidi ya Everton japo anaweza kuwepo hata
benchi katika mchezo dhidi ya Norwich na ule wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya
Schalke 04.Mchezo wa Capital League One dhidi ya Reading mwishoni mwa mwezi huu ndio
yawezekana ikawa ndio tarehe yenye uhakika zaidi ya hatimaye Wilshere kurejea
kunako kikosi cha kwanza cha washika
mitutu hao wa pale Emirates.


0 comments:
Post a Comment