 |
Mashabiki wa Senegal wakifanya vurugu |
Vurugu kubwa zilitokea katika pambano la mechi kati ya vinara wa bara la Afrika kwa ubora wa soka timu ya Ivory Coast dhidi ya Senegal maarufu kama Simba wasiofugika katika mechi ya kufuzu kwa mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini.Katika pambano hilo lililosimama kwa muda mrefu kabla ya kuvunjwa liliwashuhudia tembo hao wakiwa mbele kwa mabao 2-0 mabao yote yakiwekwa kimiani na mshambuliaji hatari wa timu hiyo ya Ivory Coast na pia nahodha wa timu Didier Drogba.
Drogba alifunga magoli hayo kwa njia ya adhabu ndogo kunako dakika ya 51 kabla ya kushuhudia tukio la kuingia uwanjani kwa shabiki mmoja katika dakika ya 61 ambaye alielekea moja kwa moja katika sehemu aliyosimama Dorgba kabla walinzi hawajamdaka na kumtoa uwanjani.
Baada ya tukio hilo mechi iliendelea na katika dakika ya 73 alikuwa tena Didier Drogba aliyewaamsha mashabiki wa Ivory Coast kwa kufunga goli la pili kwa njia ya mkwaju wa penati na hivyo kuwafanya tembo hao kuwa mbele kwa magoli 2-0 mpaka karibia na ukingoni mwa kipindi cha pili.
 |
Souleyman Bamba wa Ivory Coast na Deamba Ba wakiwa uwanjani. |
Kukiwa kumesalia dakika chache mpira kumalizika,mashabiki wa Senegal waliwasha moto jukwaani na hivyo kuzuka kwa vurugu zilizosababisha mechi hiyo kusimama kwa muda mrefu.Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinasema kuwa moto huo uliwashwa ka makusudi uwanjani kutokana na mashabiki kuchukizwa na kiwango kibovu walichoonesha nyota wao kutoka kila pembe ya dunia kama Papiss Demba Cisse,Demba Ba na Mahmadou Diame anayekipiga katika klabu ya West Ham ya nchini Uingereza.
Katika tukio hilo hakuna mchezaji yeyote aliyedhurika wakiwemo mastaa kadha wa kadha kama ndugu Kolo na Yaya Toure,Cheikh Tiote,Gervinho,Demba Ba na Cisse na wachezaji wengine.
0 comments:
Post a Comment