
Klabu ya Newcastle United imeingia mkataba na kampuni ya Wonga.com ambayo imetangaza kuidhamini klabu ya hiyo maarufu kama 'Magpies' kwa mkataba wa miaka minne.Newcastle watalazimika kuvaa Logo zenye nembo ya udhamini wa kampuni hiyo kuanzia msimu ujao wa 2012/2013.
Udhamini huo umeigharimu kampuni ya wonga.com kiasi cha fedha za Ulaya milion 1.5 ambayo ni sawa na fedha za kitanzania zaidi ya bilioni 2.Udhamini huo pia utahusisha na timu za vijana pamoja na bidhaa zitakazotengenezwa na klabu hiyo kama magari,majokofu,skafu,jezi nk

Kurudi kwa jina la St.James Park ambao unakadiriwa kuwa na uwezo wa kuchukua watu takribani 52,000 unamaanisha kuwa Newcastle United itakuwa imerudisha moja kati ya brand za klabu hiyo kwani moja kati ya sababu za klabu hiyo kujulikana sana Ulaya na duniani kote ni pamoja na uwanja wake huu wa zamani ambao wameurudisha sasa wa St.James Park.
0 comments:
Post a Comment