Hispania na Ufaransa jana zilitoshana nguvu mara baada ya kutoka sare ya magoli 1-1 huku kiungo wa klabu ya Barcelona Cesc Fabregas akikosa mkwaju wa penati.Hispania ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa beki wake Sergio Ramos na baadaye madhambi ya beki Laurent Koscielny kwa mchezaji Pedro yalizua penati ambayo ilikoswa na kiungo Fabregas.Baadaye akitokea benchi Olivier Giroud aliisawazishia Ufaransa na hivyo kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka dakika ya mwisho.
0 comments:
Post a Comment