Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Wednesday, October 31, 2012

FIFA NA UEFA NI KAMA GENGE LA WAHUNI

Wakala maarufu nchini Italia ambaye ana leseni ya kimataifa ya  uwakala kupitia Shirikisho la mpira  wa miguu Ulaya(UEFA) na lile la duniani (FIFA) Mino Raiola anayafananisha mashirikisho hayo maarufu duniani kama magenge ya wahuni na pia amekwenda mbali mpaka kumtuhumu Rais wa Shirikisho la Soka Barani Ulaya Michel Platin kama mafia.Haya yote yanakuja wakati ambapo wakala huyo anasikitika kwa mteja wake ambaye ni mchezaji maarufu sana duniani Zlatan Ibrahimovic  kushindwa kupata tuzo yoyote pamoja na kucheza soka kwa kiwango kikubwa  na huku akivichezea vilabu vikubwa kwa mafanikio kama AC Milan,Inter Milan,Juventus,Ajax Amsterdam na PSG.

Maneno ya Mino yanakuja wakati ambapo tuzo maarufu kama Ballon D'OR zikikaribia na wachezaji takribani 23 wakiwa wametajwa katika orodha ya wachezaji bora wa tuzo hiyo huku jina la Zlatan Ibrahimovic nalo likiwepo.

0 comments:

Post a Comment