Manchester United ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa nahodha wake Ryan Giggs katika dakika ya 22 kabla ya Chelsea kusawazisha kupitia kwa beki wake David Luiz kwa mkwaju wa penati mara baada ya winga wake Victor Moses kuangushwa katika eneo la hatari na beki wa pembeni Alexander Buttner.Chicharito aliifungia Man United goli la 2 katika dakika ya 43 lakini beki Garry Cahill alisawazisha kwa upande wa Chelsea katika dakika ya 52.Nani alifunga goli la tatu kwa upande wa Man United na Hazard akasawazisha kwa njia ya penati tena katika dakika ya 94 na Daniel Dturridge kufunga dakika ya 97.Dakika ya 116 Ramirez aliifungia timu ya Chelsea kabla ya Giggs kufunga kwa Man United dakika ya 120.
Mpaka pambano linaisha matokeo yalikuwa ni 5-4 Chelsea wakiibuka vinara.
0 comments:
Post a Comment