KUNDINDI A.

GNK Dinamo Zagreb VS
FC Porto
Paris Saint Germain vs FC Dynamo Kyiv.
Dinamo Zagreb na Fc Porto wameshakutama mara 4 katika
michuano hii na mara zote Dinamo Zagreb ikichomoza na ushindi na mara ya mwisho
walikutana kwenye msimu wa 1998/1999.
Paris Saint Germain na Dynamo Kyiv walikutana kwa mara
kwanza kwenye michuanao hii msimu wa 1994/95 wakati huo golikipa wa Dynamo Kyiv
Olexandr ShovkovSkiy akiwa na umri wa miaka 19 tu lakini kwa sasa akiwa na umri
wa miaka 37 akicheza mechi zote. Lakini mara mwisho walikutana kwenye robo
fainali ya michuano hii msimu wa 2008/09.
KUNDI B.

Montipellier VS Arsenal FC.
Olympiacos FC vs FC Schalke O4.
Ni kipindi cha miezi
mitatu tu tangu aondoke Stade dela Mosson
na kujiunga na Arsenal lakini michuano ya UEFA Champions League
inamrudisha Olivier Giroud nyumbani haraka kuliko alivyotarajia.Ufaransa ni
kama nyumbani kwa Arsenal hasa kutokana na ukweli kwamba sio tu ina wachezaji 7
wenye uzoefu wa ligi ya Ufaransa lakini pia ina wachezaji 6 ambao ni wazawa
bila kumsahau kocha Arsene Wenger.
Beki wa kati wa Schalke 04 Mgiriki Kyriakos Papodopolous
ameiwakilisha Olympiacos katika michuano msimu wa 2007/10.Olympiacos imecheza
michezo 6 ya kuishindani na timu kutoka Bundesliga na yamefungwa magoli 29 katika michuano hiyo ya Ulaya.
KUNDI C.

Malaga CF vs Zenit St Petersburg
AC Milan vs RSC Anderlecht.
Malaga wameshafungwa magoli 3 tu katika michezo 9
waliyocheza nyumbani kwenye mashindano haya ya Ulaya.Zenit kwa upande wao
wameshatembelea Hispania kwenye michuano hii mara 4 na wakipoteza michezo 4.
Milan kwa upande wao wanafurahia sio tu kuanza michuano hii
nyumbani lakini pia kucheza na Anderlecht kwani mara mbili walipokutana Milan
alifanikiwa kushinda na baadae kwenda kuchukua kombe.Japo kocha Allegri
anakabiriana na kibarua kigumu kwa mashabiki pale San Siro kwani wameanza
vibaya Serie A hasa michezo ya nyumbani ambako hakujawahi kuonekana zaidi ya
miaka 80. Anderlecht kwa upande wao wametembelea Italia mara 14 katika michuano
hii na hawajapata ushindi hata mchezo1.
KUNDI D.

Borrusia Dortmund vs AFC Ajax
Real Madrid CF vs Manchester City FC.
Borrusia Dortmund imekutana mara 4 na timu za Uholanzi
katika michuano na hakufanikiwa kupata ushindi mara zote .Kocha wa sasa wa Ajax Frank de Boer alikuwa kwenye kikosi
ambacho kiliifunga Dortmund kwenye robo fainali ya michuano msimu wa 1995/96.
Cristiano Ronaldo alipokuwa mchezaji wa Manchester United
ameshakutana na Manchester City katika kile kinachojulikana kama Manchester
derby mara 11 na akifanikiwa kutoka na ushindi mara 7 na kupoteza mara 3.
JUMATANO.
KUNDI E

FC Shakhtar vs FC
Nordsjaelland.
Chelsea FC vs Juventus.
Sakhtar na Nordsjaelland hawajawahi kukutana katika mechi
yoyote ya kimashindano lakini wamekutana 2011 katika mchezo wa kirafiki na
mabingwa hawa wa Ukraine Nordsjaelland wakishinda kwa 3-1.
Juventus imesafiri mara 18 kwenda Uingereza na katika mara
zote kibibi kizee cha Turin kimefanikiwa kupata ushindi mara 2 tu.Chelsea kwa
upande wao kwenye ile safari yao kwenda kuchukua Ubingwa wa mashindano haya
msimu uliopita aliifunga Napoli kutoka Italia .
KUNDI F.

LOSC Lille vs FC BATE
Borisov.
FC Bayern Munich vs Valencia CF.
BATE na Lille wote kwa pamoja wamepata wakati mgumu sana
kufika hatua ya makundi.Lille walihitaji mpaka muda wa nyongeza kuitoa FC
Kobenhvn katika mchezo wa mtoano.BATE nao mabingwa hawa wa Belarus nao
walihitaji mpaka muda wa nyongeza kuwafunga FC Vardar magoli 2 kufika hatua ya
makundi.
Bayern vs Valencia inatukumbusha fainali ya mwaka 2001
fainali ambayo Bayern walishinda kwa njia mikwaju ya penati.
KUNDI G.

FC Barcelona vs FC Spatark Moskva.
Celtic FC vs SL Benfika.
Mchezo huu utashuhudia kocha wa sasa wa Barcelona TItto Vilanova akiiongoza
timu hiyo kwa mara ya kwanza katika michuano hii akiwa kama kocha mkuu.Kocha wa
Spartak Mhispania Unai Emery atakuwa anasaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya
Barcelona akifanya hivyo mara 13 bila mafanikio.
Celtic ameshakutana na Benfica mara 2 katika mashindano haya
na mara zote walifanikiwa kufika hatua ya makundi.
KUNDI H.

Manchester United FC vs Galatasaray AS.
SC Braga vs CFR 1907 Cluj.
Kwa mara ya kwanza Garatasaray walitembelea Old Traford
ilikuwa ni msimu wa 1993/94 katika mchezo ambao uliisha kwa sare ya 3-3 na hata
hivyo hawajawahi kupata ushindi Old Trafford.
Braga na CFR hawajawahi kukutana katika michuano hii japo
CFR wana wachezaji 6 kutoka Ureno wakiwemo 3 kutoka Braga.
0 comments:
Post a Comment