
Walikuwa ni Everton walioanza kufungua akaunti ya magoli kupitia beki wake mahili wa kushoto Leinghton Baines katika dk ya 15 kabla ya mshambuliaji wa Newcastle United Demba BA kusawazisha katika dakika ya 49.Everton waliongeza goli lingine kupitia kwa Victor Anichebe dakika 88 lakini alikuwa BA tena aliyesawazisha katika dakika ya 90.
Katika pambano hilo kiungo Marouane Fellaini alinyimwa goli na mwamuzi wa akiba(mshika kibendera) kwa madai kuwa alikuwa ameotea.Hakika kwa aliyeona mechi ile alishangaa uamuzi wa mshika kibendera huyo kwani Fellaini hakuwa ameotea na hata kamera zilipolirudia lile tukio,ilionekana wazi kuwa Fellain hakuwa ameotea.Goli hilo la Fellaini limeibua mjadala mkali kati ya wadau mbalimbali hasa waandishi wa habari nchini Uingereza na wengi wao kupendekeza matumizi ya Teknolojia katika michezo yote ya Ligi Kuu ya soka nchini Uingereza.
![]() |
Sir Ferguson alikuwa mmoja wa mashuhuda |
0 comments:
Post a Comment