
Kwa wale wapenzi wa soka jumapili hii ni sikukuu manake moto
utawaka pale Etihad na pale kwenye uwanja wa Anfield.Hakika ni super Sunday ya
Manchester City vs Arsenal na Liverpool vs Manchester United kila shughuli itasimama kwa takribani masaa
3.Manake kama ni kula ule kabisa kabla ya saa 9 zaidi ya hapa unaweza usipate
kabisa hamu ya kula manake ni hatari tupu kwa wale mashabiki wa timu hizi ni patashika nguo kuchanika.Ila kwa hapa
nitatatolea macho zadi mchezo baina ya the citizen au wananchi au Manchester
City na washika bunduki wa London Arsenal pale katika dimba la Etihad hatari
tupu.
Manchester City.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya premier pale Uingereza
watapa nafasi ya kujiuliza wapi walikosea sio kwasababu walifungwa na Real
Madrid lakini swali kubwa kwa Robert Mancini itakuwa kufungwa magoli mawili
ndani ya dakika 5 pale Bernabeu.
Mashabiki wa Manchester City hawakufurahishwa kabisa na
kiwango cha Joe Hart golini hasa akilaumiwa kwa goli la Cristiano Ronaldo.Robert
Mancini baada ya mechi alimtetea Joe hart akisema wakulaumiwa ni yeye yani
Mancini kwani ndio mwamuzi wa nani asimame golini
Lakini hakika kuelekea kwenye mchezo wa jumapili lazima
ajitahidi kufuta makosa aliyoyafanya jumanne kama si hivyo atajikuta kwenye
wakati mgumu sana kwani Arsenal japo Van Persie ameondoka ila mechi dhidi ya Southampton imetuonyesha
kwamba bado wana watu wenye uwezo wa
kufunga.
Manchester City watamkaribisha Sergio Kun Aguero baada ya
kupona goti na kujumuishwa kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya Real
Madrid.Pablo Zabareta pia atarejea kikosini baada ya kupona maumivu ya
nyama.Samir Nasri atakosekana kwa majuma kaza baada ya kupata majeraha kwenye
mchezo dhidi ya Real Madrid pamoja na Mikah Richards naye ataendelea kukosekana
kutokana na matatizo ya kifundo cha mguu.
UKWELI KUELEKEA MCHEZO WENYEWE.
Manchester City wameshafungwa magoli 6 mpaka sasa katika
michezo 4 tu na kufikisha 20% ya magoli 29 waliyofungwa msimu uliopita.
Manchester City wamesharuhusu nyavu zao kutikiswa mara 13
kwenye michezo 7 katika mashindano yote
waliyocheza.
Manchester City tangu wapoteze mchezo wao dhidi ya Arsenal
mwezi wa nne msimu uliopita kwa 1-0 hawajapoteza michezo 10 mpaka sasa kwenye
ligi kuu pale nchini Uingereza wakishinda 8 na kutoa sare michezo 2.
Manchester City hawajapoteza mchezo hata 1 katika michezo 31
ya ligi waliyocheza pale Etihad wakishinda 29 ni Fulham na Sunderland pekee
ndio wamepata pointi hapa tangu mwezi wa Disemba mwaka 2010.
ARSENAL.
Arsenal kwa upande wao ilibidi wachimbe kweli kweli pale
Estadio la Mosson kupata pointi tatu muhimu za kwanza katika UEFA Champions
League.Olivier Giroud bado anatafuta goli lake la kwanza katika jezi ya Arsenal
na kitu pekee ambacho mashabiki na wachambuzi wana imani nacho kwake anahitaji
muda tu.Arsenal kwa sasa inaonekana kutengenezwa kumzunguka Santi Carzola na
mara kazaa mwenyewe akisema eneo ambalo amepewa la kucheza huru kunamfanya
ajisikie yuko nyumbani.
Kurudi kwa kiungo wa kutumainiwa Jack wilshere pamoja na
Emanuel Frimpong ,Thomas Rosicky kunamfanya Wenger awe kocha mwenye wakati
mgumu kuliko wakti wote pale Uingereza.Jack Wilshere amekosekana uwanjani kwa
miezi 14 na kurudi kwake kunanifanya niione Arsenal bora kabisa kwa kipindi cha
miezi 48 iliyopita.
UKWELI KUELEKEA MCHEZO.
Arsenal hawajafungwa michezo 9 katika mashindano yote wakishinda
4 na kutoa sare 5 na kipigo chao cha mwisho ilikuwa toka kwa Wigan mwezi wa
April msimu uliopita.
Ushindi wa Arsenal wa hivi karibuni wa 6-1 dhidi ya
Southampton ni ushindi wao mkubwa tangu waifunge Blackburn 7-1 mwezi February
msimu uliopita.
Kama Andrei Arshavin akicheza mchezo wa jumapili utakuwa
mchezo wake wa 100 wa ligi kuu nchini Uingereza.
Santi Carzola mpaka sasa ndio mchezaji ambaye ametengeneza
nafasi nyingi za kufunga kwa wenzake kuliko mchezaji mwingine yoyote kwenye
Premier ligi nchini Uingereza nafasi 14.
Mwamuzi wa mchezo wa jumapili ni Mike Dean na Arsenal
wameshinda mchezo 1 tu katika michezo 14 ambayo Amechezesha.
WALIPOKUTANA.
Arsenal wameshindwa kufunga goli kwenye michezo 5 kati ya
michezo 7 waliyokutana na Manchester City kwenye michuano yote.
Manchester City kwa upande wao wameshindwa kufunga goli hata
moja kwenye michezo 4 kati ya 5 ya ligi ambayo wamecheza na Arsenal hivi
karibuni.
Manchester City wameshinda michezo minne kati ya mitano
ambayo wamecheza na Arsenal hivi karibuni katika michuano yote.
Katika kadi nne nyekundu zilizotoka kwenye michezo minne ya
ligi kati ya Arsenal na Manchester City
kadi tatu zimeenda kwa Manchester City.
Katika mechi tatu za mwisho walipocheza msimu uliopita zote
zimeisha kwa ushindi wa 1-0
Mabingwa watetezi Manchester City wameshinda michezo 29 na
hawajapoteza hata mchezo mmoja katika michezo 30 waliyocheza pale Etihad.
Arsenal kwa upande wao wamepoteza mchezo 1 katika michezo 10
ya mwisho waliyocheza ugenini.
Tusubirie kipute cha dakika 90 pale Etihad Stadium
Hakika ni VITA YA WANANCHI NA WANAJESHI.
0 comments:
Post a Comment