Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Saturday, September 15, 2012

NI MESSI MESSI MESSI

Javier Mascherano, Álvaro Vázquez - Getafe v Barcelona
Mascherano kazini
  Akitokea benchi kama mchezaji wa akiba,mchezaji Lionel Messi jana aliendelea na rekodi yake katika klabu ya Barcelona mara baada ya kuifungia mara mbili klabu ya Barcelona katika ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Getafe katika uwanja wa Collesium Alfonso Perez.Ni ushindi wa 100% wa klabu hiyo maarufu kama 'Braugana' katika mechi nne walizocheza mpaka sasa.Iliwachukua Barca dakika 27 tu mara baada ya beki wake wa kushoto Adriano kuipatia klabu hiyo ya Barca goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza.Kipindi cha pili Barca waliongeza magoli mengine kupitia kwa Messi kwa penati dk 74 na dk 78 kabla ya kumshuhudia David Villa akiifungia pia Barca dk ya 91.Goli la Getafe lilitokana na kujifunga kwa kiungo/beki Javier Mascherano katika dk ya 80.

0 comments:

Post a Comment