![]() |
James Aspinall |
Hayo ni maneno ya mzazi anayefahamika kwa jina la Margaret Aspinall ambaye anaelezea kwa undani ni kwa namna gani maafa ya Hillsborough yalivyomgusa kwani naye alikuwa mhanga kwa kupoteza mtoto wake wa kiume James Aspinall ambaye ilikuwa ni mara yake ya kwanza kwenda uwanjani kungalia mpira.
Mama wa mtoto huyo James ambaye kwa sasa ni marehemu anatoa nasaha kwa mashabiki wa timu mbili za Liverpool na Manchester United kuwa wasije wakafanya vitendo kama vile vilivyofanywa na mashabiki miaka 23 iliyopita na kushuhudia watu takribani 96 wakipoteza maisha akiwemo James Aspinall.Tukio hilo lililotokea mwaka 1989 ambalo wapenzi wa kabumbu wanalichukulia kwa uzito mkubwa sana kutokana kupoteza watu muhimu katika medani ya soka limevuta hisia za watu wengi duniani.
Tayari watu mbalimbali wakiwemo makocha kama Sir Alex Ferguson,wachezaji,wachambuzi wa mambo wamekwisha toa matamko yao kuhusiana na tukio hilo na kusisitiza mashabiki kuwa watulivu wanapoingia uwanjani kwani matukio kama ya Hillsborough hayafai kurudia tena katika medani ya soka.Margaret anaendelea kusema kuwa"baada ya machungu ya muda mrefu,nawaomba mashabiki wasije kuruhusu matukio yanayo fanana na Hillsborough kujirudia.Familia zote 96 ambazo zilipoteza ndugu,jamaa au marafiki wanahitaji kufarijiwa na si kusikia kitu kama kile kikitokea tena".

Akiendelea kusimulia tukio la kufa kwa mwanaye James,Margaret anasema"James alienda uwanjani majira ya alasiri kama saa (1:20pm) kwa saa za Uingereza ambayo ni saa 9 na dk 20 kwa saa za Afrika Mashariki .Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kwenda uwanjani na alikuwa na shauku ya kwenda uwanjani siku hiyo.Lakini cha kustaajabisha ni kuwa alirudi akiwa katika jeneza."
Ningependa kutoa ushauri kwa mashabiki wa timu za Liverpool na Manchster United kuwa watulivu hasa katika mchezo wao wa kesho.Hakuna sababu ya kufanya vurugu kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha ya watu wengi anasema Margaret.Nawaasa pia vyombo vya usalama kuwachukulia hatua wale wote watakohusika na uvunjifu wa mani katika viwanja vya michezo hasa mpira wa miguu.
Margaret anamalizia kwa kusema kuwa mpira wa miguu hauna uadui bali ni ni mchezo wa furaha.Uhasama upo lakini si wa kufanyiana vurugu au kugombana.Mpira wa miguu ni wa upendo na furaha kwa watu wote bila kuangalia umri.

Margaret Aspinall
0 comments:
Post a Comment