
Haya ni maneno ya kocha wa 'The Braugana'Tito Vilanova wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea pambano lao la leo katika ule mfululizo wa Ligi Kuu ya soka nchini Hispania maarufu kama La Liga."Ni mchezaji bora duniani kama si mchezaji bora katika historia ya mpira wa miguu duniani.Na kwa mashabiki wa klabu ya Barcelona watakuwa na furaha kumuona mchezaji huyo akimalizia soka lake katika klabu hiyo ya Catalunya".
Klabu hiyo ya Catalunya itajitupa uwanjani leo kupambana na klabu ya Granada katika ile mwendelezo wa Ligi Kuu ya soka nchini Hispania.Kocha Vilanova ataendelea kuwakosa baadhi ya nyota wake kama nahodha Carles Puyol na Gerad Pique katika sehemu ya Ulinzi na anafikiria kuwapanga viungo Alex Song na kinda Marc Bartra katika sehemu hiyo ya ulinzi."Nitaamua nani acheze kama ni Marc Bartra ambaye amekuwa ni sehemu ya timu na anastaili kucheza au Alex Song kwani naye ana uzoefu kidogo katika sehemu hiyo"alisema Vilanova.
0 comments:
Post a Comment