
Klabu ya Barcelona inafikiria kumuongezea mkataba mpya mchezaji wao nyota Lionel Messi ambao utamfu nga kwa muda mrefu hapo Camp Nou.Akizungumza na kituo cha radio cha Catalunya,Rais wa klabu hiyo anasema kuwa"tunafikiria kumuongezea mapema mkataba mpya mchezaji wetu Lionel Messi ambao utamfanya kuendelea kuwa mmoja kati ya wanafamilia wetu.Tunamhitaji Messi na yeye pia anatamani kumalizia soka lake hapa kwetu hivyo ni dhahiri kuwa kumpa mkataba mpya ni kumtendea haki na kuendelea kuwa naye katika klabu yetu hii."Messi ambaye mkataba wake wa sasa unakwisha mwaka 2016 amekwisha wahi kusema kuwa angependa kumalizia soka lake katika klabu hiyo ya Barcelona.Katika hatua nyingine mchezaji huyo alikuwa nyota wa mchezo katika pambano la jana katika ule usiku wa Ulaya dhidi ya timu ya CSKA Moscow ya Urusi mara baada ya kufunga mara mbili katika raundi ya kwanza ya klabu bingwa Ulaya huku Barcelona wakiibuka na ushindi wa magoli 3-2.
0 comments:
Post a Comment