
Ilikuwa ni mechi nzuri sana na ya kusisimua ambayo iliwakutanisha mabingwa wa zamani wa Escudetto klabu ya Associazione Calcio Milan(AC Milan) dhidi ya Atalanta Bergamo katika dimba la San Siro pale katika kitongoji cha Lombard kunako jiji la Milan.Walikuwa ni vijana wa kocha Stefano Colantuono nawazungumzia Atalanta Bergamo ambao waliwaduwaza Milan kwa kuwafunga goli moja kwa bila.Goli la Atalanta lilifungwa na mmoja kati ya viungo bora kabisa katika Serie A Luka Cigarini katika dk ya 64.Milan bado walionekana kukosa umakini katika ulinzi na hivyo kuleta wasiwasi wa kuwa kama wataweza kuleta changamoto kwa mabingwa watetezi klabu ya Juventus.Bado mzimu wa mabeki hodari walioondoka kunako klabu hiyo nawazungumzia Thiago Silva na Alessandro Nesta unaendelea kuwagharimu kutokana na safu ya ulinzi ya klabu hiyo inayoundwa na Francesco Acerbi,Daniele Bonera,Ignazio Abate na Luka Antonini kushindwa kuelewana vizuri.Bado pia kuna tatizo kwa kocha Massimiliano Allegri katika kuchagua kikosi cha kwanza cha timu hiyo.Kuwekwa benchi kwa wachezaji kama Mattia De Sciglio,Mathew Flamini na Antonio Nocerino kuliigharimu timu hiyo hasa katika sehemu ya kiungo kwani sehemu hiyo ilishindwa kuwa na ubunifu na hivyo kupelekea safu ya ushambuliaji kupwaya kutokana na kukosa mipira mara kwa mara.Milan walipoteza mechi ya pili katika mechi tatu walizocheza kwani tayari walishapoteza mechi na Sampdoria katika ufunguzi wa pazia la Serie A nchini Italia.

Kunako uwanja wa Renzo Barbera klabu ya Palermo ililazimishwa sare ya 1-1 na klabu ya Cagriali katika mwendelezo wa Serie A ikiwa ni raundi ya tatu ya Ligi hiyo ya nchini Italia.Walikuwa ni vijana wa kocha mpya wa timu hiyo ya Palermo Pepe Sannino walioanza kuziona nyavu za Cagirali kupitia kiungo mkakamavu Egidio Alevaro Rios katika dk ya 41 kabla ya Marco Sau wa Cagriali kusawazisha katika dk ya 88.
0 comments:
Post a Comment