Ni UEFA SUPER CUP tena tarehe 31/8/2012 majira ya saa 3:30 za huku kwetu Afrika mashariki linafanyika katika jiji la Monaco nchini Ufaransa katika Uwanja wa Stade de Lois 11 na ni Ijumaa baada ya swala kabla ya sabato hatari kweli kweli.Pambano linalowakutanisha mabingwa wa UEFA champions League na mabingwa wa UEFA Europa league Chelsea na Atletico Madrid kwa pamoja.Hakika ni pambano ambalo tumia mizani yeyote unayohisi itafaa kupima umuhimu na uzito wa pambano lenyewe bado jibu litabaki moja tu la kuwaahidi mashabiki kote duniani pambano kali na kuvutia kweli kweli.Chelsea wakiwa wapya kabisa na wanaovutia kutazama kwa sasa nina uhakika mpaka ikifika katikati ya msimu huu Roman Abramovich anaweza kumualika kipenzi ama watoto mjini wanasema kali yake Dasha Alexandrovna Zhukova kuja kuangalia maajabu ya Eden.
Ni pambano kati ya The Blues vs Los Rojiblancos au Red and Whites,Spain vs England, Torres vs Falcao,Cech vs Courtois na Mwisho kabisa ni pambano kati ya vijana makocha Diego Simeone na Robert Dimateo ambao wote wamechezea vilabu hivi kwa mafanikio makubwa kwelikweli.Pambano hili linamrudisha Dimateo tena Monaco katika fainali ya Supercup wakati ule 1998 Chelsea wakiifunga Real Madrid 1-0 kwa goli la Gustavo Poyet lakini leo akirudi tena kama kocha.Diego Simeone naye baadae 1999 akishinda Supercup na S.S Lazio kwa hiyo wote kila mmoja anatamani kuandika historia nyingine.
Chelsea wakiongoza msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza kwa sasa kocha wao Robert Dimateo anasema “ Ni vizuri kushinda kombe lingine la kimataifa kwaajili ya timu hii na tunafurahi tunaeleka kwenye mchezo huu tukiwa tumeshinda michezo mitatu ya ligi na kila mtu anaonekana yuko fiti” anaendelea anasema mechi hii sio ya kirafiki kuna kombe uwanjani na tunataka kushinda kwa hiyo tunaichukulia kwa uzito mkubwa sana na hatutopumzisha mchezaji hata mmoja”.Atletico Madrid au Los Rojiblancos wenyewe kwa sasa wanakamata nafasi ya nne na pointi zao 4 kocha wao Diego Simeone nao wanaonekana wako tayari.
Kazi kubwa ya Peter Cech na ukuta mzima wa Chelsea kama wanataka kweli kulipeleka kombe hili pale kaskazini mwa London lazima wahakikishe Ledamel Falcao Garcia anakuwa na usiku mbaya.Huyu jamaa ni zaidi ya hatari ni moja kati ya washambuliaji bora wa kati kwa sasa diniani kama sio Christiano Ronaldo au Lionel Messi hakika kile kiatu cha mfungaji bora wa La Liga ni cha kwake na hata namuona na nadiriki kusema ni mkubwa sana kuliko Atletico Madrid. Msimu uliopita wa La Liga alifunga magoli 24 anahitaji kuondoka kwenda kwenye timu kubwa zadi ni mfungaji bora wa UEFA Europa ligi mara mbili mfululizo akifanya hivyo akiipa FC Porto kombe msimu wa 2011 na 2012 akifanya tena vitu vya hatari na kuwapa Atletico Madrid kombe.
0 comments:
Post a Comment