![]() |
Paul Pogba |
POGBA
AELEZA KILICHOMKIMBIZA MAN UTD.
Mchezaji chipukizi wa zamani wa Manchester United
Paul Pogba aliyejiunga na klabu ya Juventus ya nchini Italia msimu huu ameeleza
sababu ya yeye kuondoka katika klabu ya Manchester United na kuhamia
Juventus.Akizungumza na gazeti la L’Equipe Pogba mwenye umri wa miaka 19 anasema,”sijutii
uamuzi wangu wa kuondoka Man Utd
analiambia gazeti la L’Eqipe.Nimejifunza mengi nikiwa na Man Utd lakini watu
inabidi wanielewe na wauelewe uamuzi wangu.
Kocha Sir Alex Ferguson aliniamini sana lakini
hakunipa nafasi ya kucheza na alikuwa akinieleza kuwa bado ni mdogo sana na
hivyo niwe na subira kwani muda wangu wa kucheza utakuja ingawa haikuwa
hivyo.Pamoja na kuwa alikuwa ni bosi wangu lakini ndoto yangu ilikuwa bado ni
kucheza mpira kila mara katika kikosi cha Man Utd.
Nilipofika hapa Juventus,kocha Antonio Conte
aliniambia wazi kuwa alikuwa anataka mchezaji wa kucheza pahala pa Pirlo pamoja
na Vidal katika kikosi cha kwanza mana timu itashiriki michuano mingi na
mikubwa hivyo anahitaji kuwa na mzunguko wa wachezaji katika idara ya kiungo.Pogba
hakusita pia kuzungumzia kauli ya kocha wake wa zamani Ferguson yakuwa hakuwa
na nidhamu kwa kusema’kauli ya kocha Ferguson ilinishangaza sana mana sikuwai
kumkosea adabu Sir Alex ingawa kuna baadhi ya mambo tulishindwa kuelewana’.”
0 comments:
Post a Comment