BALOTELLI KUWAKOSA ENGLAND...........
Mshambuliaji
wa klabu ya Manchester City ya nchini England Super Mario Balotelli ameondolewa
katika kikosi cha timu ya taifa ya Italia baada ya kugundulika kuwa na matatizo
ya macho.Timu ya taifa ya Italia maarufu kama Azzuri itacheza mchezo wake wa
kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya England siku ya tarehe 15 mwezi huu wa nane
pale nchini Uswisi kama kalenda ya FIFA inavyosema.
Balotelli
ambaye pia alishindwa kucheza katika pambano la Ngao ya Jamii siku ya Jumapli
iliyopita dhidi ya Chelsea,atarudi uwanjani kama kawaida katika katika mechi za
ligi kuu ya soka nchini England zinazotarajiwa kuanza mwishoni mwa juma hili.Katika
kikosi cha Italia kilichotajwa na mwalimu Claudio Prandelli,wachezaji chipukizi
wamepewa sana nafasi na zaidi ni klabu ya Atalanta kutoa wachezaji watatu
katika kikosi hicho cha Azzuri.
Wachezaji hao ni
pamoja na mshambuliaji Manolo Gabbiadini,beki Federico Peluso na golikipa
Andrea Consigli.
Vikosi vya timu
za zote ni hivi hapa
Kikosi cha Italia
Andrea Consigli
(Atalanta), Mattia Perin (Genoa), Salvatore Sirigu (Paris St Germain); Ignazio
Abate (AC Milan), Francesco Acerbi (AC Milan), Davide Astori (Cagliari),
Federico Balzaretti (Roma), Mattia De Sciglio (AC Milan), Daniele Gastaldello
(Sampdoria), Angelo Obinze Ogbonna (Torino), Federico Peluso (Atalanta);
Alberto Aquilani (Fiorentina), Daniele De Rossi (Roma), Alessandro Diamanti
(Bologna), Antonio Nocerino (AC Milan), Andrea Poli (Sampdoria), Ezequiel
Schelotto (Atalanta), Marco Verratti (Paris Saint Germain); Mario Balotelli
(Man City), Mattia Destro (Roma), Stephan El Shaarawy (AC Milan), Manolo
Gabbiadini (Atalanta
Kikosi cha England
Magolikipa: Joe Hart (Manchester City), Jack Butland (Birmingham
City), John Ruddy (Norwich City).
Mabeki: Leighton Baines (Everton), Ryan Bertrand (Chelsea),
Gary Cahill (Chelsea), Steven Caulker (Tottenham Hotspur), Phil Jagielka
(Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur).
Viungo: Michael Carrick (Manchester United), Tom Cleverley
(Manchester United), Frank Lampard (Chelsea), Adam Johnson (Manchester City),
Jake Livermore (Tottenham Hotspur), James Milner (Manchester City), Alex
Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Jack Rodwell (Everton), Ashley Young (Manchester
United).
Washambuliaji: Andy Carroll (Liverpool), Jermain Defoe (Tottenham
Hotspur), Daniel Sturridge (Chelsea), Theo Walcott (Arsenal).
0 comments:
Post a Comment