Wednesday, August 22, 2012
LIGI KUU UINGEREZA: CHELSEA YAIFUNGA READING
Posted on 2:30 PM by Unknown
Klabu ya Chelsea imeendeleza wimbi la ushindi katika mfululizo wa mechi za Ligi kuu ya soka nchini Uingereza.Katika mechi iliyoisha hivi punde Chelsea imeibuka na ushindi mnono wa magoli 4-2 dhidi ya timu iliyopanda daraja ya Reading.Alikuwa ni Eden Hazard tena ambaye ameonesha ni kwa namna gani klabu hiyo ya Chelsea haikukosea kumnunua kwa kitita cha takribani(euro 32m) akitokea klabu ya Lille Metropole ya nchini Ufaransa.Hazard aliweza kutoa pasi mbili za magoli kwa Gary Cahill dk ya 69 na Ivanovic dk ya 90+5 huku magoli mengine yakifungwa na Frank Lampard kwa mkwaju wa penati na lingine likifungwa na Fernando Torres.Magoli kwa upande wa Reading yalifungwa na Pavel Pogrebnyak dk 25 na Danny Guthrie dk 29.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment