
Jina lake kamili alilopewa na wazazi wake pale mitaa ya Kaduna Nigeria baada ya kuzaliwa tarehe 12/12/1990 ni Victor Moses. Huyu jamaa ni hatari sana na hakika mtu ambaye ameshamsumbua sana Dimateo kumsajili Moses baada ya ule ushindi wa 2-0 pale Stanford Bridge baina ya Chelsea na Wigan ni Ashly Cole. Nina uhakika jamaa alilala na viatu manake ameshika sana jezi huyu mtu ana kila kila lakini silaha yake kubwa nguvu na kasi hakika alikuwa ni mkubwa kuliko Wigani.Ana uwezo wa kucheza namba tofauti winga na hata mshambuliaji wa pili ila Wigan amecheza sana winga.Mnamo tarehe 23-8-2012 Wigan walimpa Moses nafasi ya kuzungumza na Chelsea masula binafsi na tarehe 24 -8-2012 katika mtandao wa Chelsea wakatangaza kumnasa mchezaji huyo kwa ada ya
£7mil na baadae kuongezea £2mil.
 |
Moses vs Obi Mikel |
Azaliwa Nigeria lakini katika umri wa miaka 11 akahamia Uingereza na wazazi wake na kujiunga na Crystal Palace lakini katika msimu wa 2009-2010 katika dirisha dogo la usajili mwezi kwanza Wigan walimsajili kwa ada ya
£2.5mil baada ya Crystal Place kupata matatizo ya kiutawala.Mechi yake ya kwanza ilikuwa ni ya sarte ya 1-1 na Sunderland na alikuja kufunga goli lake la kwanza dhidi ya Hull City tarehe 3-5- 2010.
TIMU YA TAIFA.
 |
Moses | |
Japo amezaliwa Nigeria lakini Moses ameviwakilisha vikosi vya Timu ya taifa ya Uingerza vya umri mbali mbali kama chini ya miaka 16,17,18,19,21 lakini alikuja kuchagua kucheza timu ya taifa ya wakubwa ya Nigeria bdala ya Uingereza kwani sheria za FIFA zilkuwa zina mruhusu. Aliitwa kwa mara kwanza Super Eagkles mwezi wa pili 2011 katika mechi dhidi ya Guatemala lakini mechi hiyo ya kirafiki ikaahirishwa.Mwezi wa tatu naliitwa tena kwenye mechi hdidi ya Ethiopia lakini haucheza baada ya kibali chake kuchezea Super Eagles kuchelewa.Mnamo tarehe 1-11-2011 FIFA walitangza kibali cha Moses kuwa tayari na aliichezea Super Eagles mchezo wa kwanza katika mechi dhidi ya Rwanda akiingia kipindi cha pili tarehe 29-2-2012.
0 comments:
Post a Comment