Hatimaye Fabrice Muamba amemua kuachana na soka baada ya ushauri kutoka kwa
jopo la madaktari.Muamba alipata tatizo la moyo pale uwanja wa White Hat Lane
kwenye mchezo wa kombe la FA baina ya timu yake ya Bolton Wonderes na Tottenham
Hotspurs mwezi wa tatu. Moyo wa Muamba ulisimama kwa takribani dakika 78 kabla
ya timu ya madaktari kufanya kazi ya ziiada pale uwanjani kabla ya kupelekwa
Hospitali kwa matibabu zaidi.Baada ya kukaa nje kwa takribani mwezi mmoja hali
ya Muamba ilikuwa inaendelea kuimarika siku hadi siku na kukawa na matumaini kwamba
angeweza kurejea uwanjani hivi karibuni.
Wiki iliyopita Alisafiri kwenda Ubelgiji kukutana na daktari
wa masuala ya moyo na akashauriwa kutokana na hali ya moyo wake hawezi
kuendelea kucheza tena mpira.Kabla ya kutangazwa rasmi kwa taarifa hiyo Muamba
ailiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba”Watu waendelee
Kutabasamu”.Muamba alifika England akitokea Kongo na kunza maisha yake ya soka
na klabu ya Arsenal kabla ya kwenda Birmigham na baadae Bolton Wonderes.Muamba
alicheza pia kwenye vikosi tofauti vya timu za Taifa za vijana Uingereza kabla
ya haya maamuzi yake ya kustaaafu soka.
0 comments:
Post a Comment