Quintel Blogger theme

A free Premium Blogger theme from newbloggerthemes.com

Tuesday, September 4, 2012

JACK WILSHERE AKARIBIA KABISA KUTUA EMIRATES


Huku dirisha la usajili likiwa limemalizika na kufungwa barani Ulaya dirisha la Arsenal bado liko wazi huku wakikaribia kabisa kumnasa kiungo mmoja na beki mmoja. Baada ya kuondokewa na Alex Song pamoja ana RobinVan persie waliokwenda Barcelona na Manchester United kwa pamoja Arsenal bado inaonekana ipo sokoni na kocha Arsene Wenger ameweka wazi dhamira yake ya kutaka kukiimarisha kikosi chake.Baada ya kuwasajili Lukas Poldoski, Santi Carzola pamoja ana Olivier Giroud Wenger aliwaeleza mashabiki kwamba bado atasajili beki mmoja na kiungo mmoja amabao ni Jack Wilshere pamoja na Bacary Sagna.

Arsene na Arsene wenger wanaweza kupokea habari nzuri unaweza kusema kuliko zote hasa katika kipindi hiki baada ya Jack Wilshere kuanza kupangiwa mazoezi mfululizo  ya mpira akitikoka katika mazoezi ya Kujenga mwili na kuiimarisha misuli yake  iliyokuwa imepatwa na majerha.Jack Wilshere amekekaa nje ya uwanja kwa takribani miezi 12 sasa na kurejea kwake ni faaraja sio kwa Arsene Wenger pekee bali pia hata kwa kocha wa kikosi cha timu ya taifa Roy Hogson.

Baada ya kumaliza wiki ya mazoezi na mpira Wilshere anatarjiwa kucheza michezo mitatu na timu ya wachezaji wa akiba kabla ya kurejea kabisa kwenye pilikapilika na kikosi cha kwanza kuilisaka taj lilokosekana Emirates kwa msimu wa 7 sasa  mwishoni mwa mwezi huu. Arsenal pia inachagizwa na kurejea kwa beki wake kulia wa kutumaniwa Bacary Sagna mwishoni mwa mwezi huu baada ya kukosekana kwa



 takribani miezi 4 alipovunnjika mguu mwezi Mei katika mchezo dhidi ya Norwich City.

0 comments:

Post a Comment